MH.BENDERA ATEMBELEA WILAYA YA ULANGA KUANGALIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KATIKA BONDE LA KILOMBERO
JAMII 5:52 AM
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akionesha mpaka kati ya Kijiji cha Igawa, Malinyi na Pori Tengefu la Bonde la Kilombero, ambapo wananchi wamevamia kwa kulima na kufanya malisho ya mifugo yao.
Diwani wa Kata ya Malinyi , Said Tira wa Chadema ( kulia) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera ( kati) huku Diwani mwenzake wa CCM Kata ya Igawa,Severus Kamguna, akisikiliza kwa makini
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera, (mwenye miwani) akifuata nyayo za RPC Adolfina Chialo aliyeongoza mstari, kwenda kuangalia uharibifu wa Bonde la Kilombero.
Mifugo nayo ndani ya Pori Tengefu la Bonde la Kilombero
Makazi ya jamii ya wasukuma ndani ya Pori Tengefu, Bonde la Kilombero
Gari la Polisi , Wilaya ya Ulanga, likiwa limenasa kwenye tope , ndani ya mashamba yaliyolimwa katika Bonde la Kilombero.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Igawa, Tarafa ya Malinyi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (hayupo pichani), wakati alipotoa amri ya kuzuia shunghuli za kilimo na ufugaji katika bonde la Kilombero.
Baadhi ya wakulima wa Wilaya ya Ulanga waliovamia bonde la Kilombero , wakirejea baada ya kupata maekelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera ( hayupo pichani).
Baadhi ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kisukuma, wakitoka mashambani ili kumsikiliza Mh. Bendera (hayupo pichani).
Sehemu ya Mashamba makubwa yaliyilimwa ndani ya Pori Tengefu katika Bonde la Kilombero, eneo la Maguba, Malinyi , Wilaya ya Ulanga