MKUU WA WILAYA YA KOROGWE AKARIBISHA WAWEKEZAJI WENYE NIA YA KUJENGA HOTELI KUBWA WILAYANI HUMO


Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima, akiweka jiwe la msingi katika MGAHAWA wa Rock Hill Rest uliopo katika barabara kuu ya Korogwe/Same katika kijiji cha Kiloza ambao ni maalumu kwa ajili ya wasafiri wanaotumia barabara ya Kasakazini yenye mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima, akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi katika MGAHAWA wa Rock Hill Rest mara baada ya kuweka jiwe hilo la msingi, anayefuata baada ya Mkuu wa wilaya ni Mkurugenzi wa Mgahawa huo Bw. Estomio Urio na wengine ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Korogwe.
Wafanyakazi na wadau wakubwa wa mtandao huu, wakiwa wameandaa chakula tayari kwa wateja wao watakaofika hapo iwe ni kwa mabasi makubwa au magari madogo.
Eneo la mgahawa wenyewe unavyoonekana ukiwa chini ya mlima wa Lutindi ambao umekuwa ukileta upepo kwa wasafiri wanaofika kupata chakula katika mgahawa huo.

Katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima aliendelea kuita wawakezaji katika wilaya hiyo ambao wataweka migahawa mikubwa na hoteli katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia kutoa ajira na pia ulipaji wa kodi kwa serikali.

Alisema suala la uwekezaji kama huo ni muhimu lakini pia aliwaasa wawekezaji wanaowekeza miradi mikubwa kama hiyo kuishi vizuri na wananchi wanaozunguka maeneo hayo ikiwemo kusaidia huduma za jamii katika eneo hilo badala ya wawekezaji kuzalisha migogoro.

Mmiliki wa mgahawa huo mzuri Bw. Urio alisema anaishukuru benki ya CRDB kwa kumwezesha kumpatia mkopo ambao umemfanya aweze kujenga mgahawa huo katika kipindi cha mwaka mmoja kwa gharama ya shilingi milioni 800 hadi sasa ukiwa umefikia awamu ya kwanza ambapo anatarajia kujenga hoteli na kuimalizia katika awamu ya pili anapotarajia kutumia shilingi bilioni 1,6 hadi kukamilisha mradi wake huo.

Mgahawa huo wa chakula kwa wasafiri kwa barabara hiyo unakuwa ni wa Nne mkubwa baada ya ule wa Liverpool uliopo eneo la Mombo, Mombo Resort, Dar Express (Highway Resort) na huu sasa Rock Hill Rest.

Posted by Bigie on 11:12 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.