NELLY KAMWELU AINGIA 5 BORA KATIKA SHINDANO LA MISS TOURISM QUEEN INTERNATIONAL 2011/2012
JAMII 11:12 PM
Nelly Kamwelu ambaye ni mshindi wa Miss Universe Tanzania 2011 (wa kwanza kushoto)ameingia katika 5 bora ya mashindano ya utalii ya Miss Tourism Queen International 2011/12 yaliyofanyika nchini China mji wa Xian.
Nelly ameshika nafasi hiyo mbele ya warembo wengine 92 katika shindano hili ambalo ni la 5 kwa ukubwa duniani.
Mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International alikuwa Mrembo wa Thailand, mrembo wa Fernando de Noronha alishika nafasi ya pili, Belarus nafasi ya tatu na mrembo wa China ashika nafasi ya 4. Nelly anarejea nchini tarehe 29 na ndege na Emirates.