MUONEKANO WA JIJI LA DAR ES SALAAM MCHANA HUU BAADA YA MVUA YA JANA....
JAMII 5:06 AM
Daraja la Luhanga limekatika na watu wanapita katika maji yenye kimo cha kiunoni
Dar na foleni ya asubuhi.Hapa ni njia panda ya tabata segerea na foleni hii imeanzia Buguruni
Godoro limenasa kwenye mti.Limeletwa hapo na maji jana
Watu wakipata shida kutembea kwani maeneo mengi mitaani yamejaa maji
Ukuta wa shule ya msingi Gonzaga Luhanga umebomolewa na maji jana
Leo Ubungo maziwa.Maduka,bucha na saloon vikiwa vimefungwa na maji yamejaa ndani
Mti mkubwa umeng'olewa na kuangukia nyumba hivyo kusababisha uharibifu mkubwa,Mabibo
Familia zikihangaika kumalizia usafi katika nyumba zao.Samani hizi hasa masofa yameharibiwa kabisa
Mabibo,nyumba zimeharibiwa na maji ya mto
Kigogo mwisho, baadhi ya vitu vya familia ambazo bado hazijapata ufumbuzi juu ya makazi yao
Mzee huyu anaendelea na usafi wa nyumba yake maeneo ya Luhanga
Luhanga, hapa watu wamelala usiku wanapaita camp baada ya kuwa wameshindwa kumaliza kutoa tope katika nyumba zao
Daraja la kigogo limekatika.vijana wameweka nguzo za umeme na wanatoza 500 kwa kila anayepita hapo.anayeogopa kuvuka mwenyewe wanamsaidia kuvuka kwa sh 1000.
Hapa vijana wakimsaidia dada kuvuka
Nyumba zaidi ya 4 zimeharibiwa kabisa maeneo ya kigogo darajani,wakazi wanajaribu kutoa mabaki ya matofali
Huyu bwana kaamua kuchukua tahadhari mapema.Anahama tabata dampo