"ORIJINO KOMEDI IMENITOA KIMAISHA"--MPOKI
JAMII 11:19 PM
MCHEKESHAJI wa kundi la Orijino Komedi, Mpoki amefunguka na kusema kuwa fani hiyo imeweza kumtoa kimaisha na anaishukuru kwa sababu ni moja ya kazi ambazo zimeweza kuonesha nyota katika maendeleo yake.
Alisema kupitia Komedi ameweza kujenga nyumba ya kuishi na kuwa na usafiri wake vitu ambavyo awali hakujua kama angeweza kuvipata ingawa malengo yake yalikuwa ni kuja kumiliki vitu hivyo pamoja na kuishi ndani ya nyumba yake.
Alisema hata hivyo bado anahitaji kutoka zaidi kimaisha ingawa kwa sasa amefanikiwa kwa kiasi fulani kitu ambacho kila siku amekuwa akimshukuru mungu kwani kumpa kwani wapo wengine wamekosea.
“Komedi ni fani ngumu sana kwani kumfanya mtu aliyenuna acheke siyo kitu kidogo hivyo hata tuna magari basi tumshukuru mungu kwani ametupa vipaji kwa malengo yake, lakini naweza kusema kwamba kama mimi nimepewa hiki basi kuna mwingine kapewa kingine ambacho mimi sina,” alisema.
Mbali na uchekeshaji pia msanii huyo anauwezo mkubwa wa kuimba staili yoyote ikiwemo ya mashairi ambapo wimbo wake unasikika ni ule aliomjibu Mrisho Mpoto wa ‘Shangazi’, huku wa Mpoto ukiwa ni ‘Mjomba’