"NIMPENDE NANI KATI YA WEMA NA JOKATE?????????" ---DIAMOND
JAMII 10:09 PM
WAKATI bifu ya mrembo Jokate Mwegelo na Wema Sepetu ikiendelea kuchukua sura mpya kwenye vyombo vya habari bongo, mkali wa bongo flava Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameachia track inayokwenda kwa jina la "nimpende nani" .
Diamond ametoa ngoma hiyo kama swali kwa mashabiki wake kutokana na hali halisi ya sakata hilo inavyoendelea kwa sasa kwani wiki chache zilizopita aliachia ngoma nyingine mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mawazo’ ambao ndo kwanza imeanza kushika kasi katika vituo mbalimbali vya redio.
Kwenye wimbo huo Diamond anaonekana kujiuliza ampende nani, huku akiwataja kwa majina Wema na Jokate, huku singo hiyo ikiwemo ndani ya albamu yake aliyoingiza sokoni mwezi Novemba iitwayo ‘Lala Salama’ ambapo sehemu ya mashairi ya wimbo huo inasema “Yasiwe kama ya Wema sepetu kila siku magazeti, simtaki kama Uwoya ni mtemi anahasira,awe mpole kama Jokate, Sauti kama Wema akiwa analia, Kicheko kama cha Fetty…nimpende nani, nimpendeee”.
Albamu hiyo ina nyimbo kama ‘Moyo Wangu’ ambao ulipata kushika chati mbalimbali za muziki, pia kuna ‘Lala salama’ uliobeba jina la albamu, ‘Chanda chema’, ‘Nimpende nani’, ‘Najua’, ‘Mawazo’, ‘Kwanini’, ‘Gongolamboto’, ‘Natamani’ na ‘Kizaizai’.