SHAMSA AFANYIWA KITU MBAYA NA VIBAKA WA MLIMANI CITY
JAMII 5:13 PM
MREMBO anayetikisa vilivyo ndani ya Bongo Movies ,Shamsa Ford alifanyiwa kitu mbaya na kuonja joto ya jiwe baada ya wahuni kuvunja gari lake na kumuibia vitu mbalimbali vya thamani.
Habari kutoka kwa shuhuda wetu, zinasema kwamba tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita, Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo Shamsa alikwenda hapo na mchumba wake aitwaye Dick kuhudhuria harusi ya rafiki yao.
“Walipofika hapo waliegesha vizuri na kuingia ukumbini, lakini huku nyuma wahuni wakavunja kioo cha nyuma na kuwaibia,” kilieleza chanzo hicho.
Aliendelea kunyetisha kuwa, baada ya sherehe kuisha na wawili hao kutoka kwa lengo la kwenda nyumbani, ndipo walikuta kioo cha nyuma kimevunjwa na baadhi ya vitu vyao havipo.
Baada mpekuzi wetu kunasa habari hiyo,alimpandia hewani Shamsa ili aweze kuelezea kilichotokea, ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha.
“Ni kweli tuliibiwa. Nilikuwa na Dick (mchumba wake) kwenye harusi pale Mlimani City, wakati wa kutoka, tukakuta kioo cha nyuma kimevujwa. Wamechukua vitu vingi sana, pamoja na pesa kiasi cha shilingi milioni moja,” alisema Shamsa kwa uchungu na kuongeza:-
“Nawachukia sana wezi kwa kweli, nikikuta mwizi anapigwa mahali, nitachukua chochote kitakachokuwa mbele yangu nimpige. Wanarudisha watu nyuma, yaani sina amani nao kabisa.”
