SIMU YAMLIPUA MFANYABIASHARA
JAMII 10:05 PM
Mbunge wa jimbo la Ludewa Mhe.Deo Filikunjombe akimjulia hali mfanyabiashara huyo baada ya kutembelea Hospital ya wilaya ya Ludewa kuona na kutoa misaada mbali mbali kwa wagonjwa .
Mfanyabiashara huyo anadai chanzo ni simu ya mkononi kulipuka na moto kushika Petrol baada ya chumba chake cha kuhifadhia mafuta ya biashara kushika moto ambao chanzo chake ni simu hiyo kulipuka .
Imeelezwa kuwa wakati wasamaria wema wakijaribu kunusuru nyumba kuteketea kwa moto waliamua kuchukua ndoo moja ambayo ndio ilikuwa imeshika moto huo na kuitupa nje na ndipo ilipo mkuta mwilini mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa akikimbilia kusaidia kuzima moto huo.