TACAIDS YATOA ZAWADI KWA WAANDISHI WA HABARI ZA UKIMWI HAPA NCHINI
JAMII 3:43 AM
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho(kushoto ) akitoa cheti na cheki ya shilingi laki saba kwa mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Renatus Mutabuzi wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho(kushoto ) akiongea na waandisha wa habari jana jijini Dar es salaam wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za UKIMWI nchini (AJAAT) Simon Kivamo na kulia ni Afisa Uraghibishi (Advocacy Officer) wa TACAIDS Simon John.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za UKIMWI nchini (AJAAT) Simon Kivamo(kulia) akiongea na waandisha wa habari jana jijini Dar es salaam wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache . Kushoto ni Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho.