UWOYA AJIKUTA AKIMWAGA MACHOZI BAADA YA MUMEWE NDIKUMANA KUTOROKA NA MTOTO WAO

Msanii   wa filamu Bongo, Irene Uwoya amejikuta akisherehekea Sikukuu ya Chrismasi kwa machungu kufuatia mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kutoweka na mtoto wao Krish katika mazingira ya kutatanisha.


Akizungumza kwa njia ya simu na mpekuzi wetu Jumamosi ya Desemba 24, mwaka huu, Irene alisema mpaka siku hiyo alikuwa hajui aliko Ndikumana na mtoto wao, hali iliyomfanya achanganyikiwe.


Alisema: “Mimi na Ndikumana tunakaa Sinza, jana asubuhi (Ijumaa iliyopita) yeye (Ndikumana) aliamua kwenda kumuangalia mtoto ambaye siku zote anakaa na bibi yake huko Mbezi.


“Alipofika alimkuta msichana wa kazi, mama hakuwepo, yule msichana akamuachia mtoto na kwenda gengeni, hapo ndipo Ndikumana alipoondoka na mtoto na kuanzia siku hiyo hakurejea Mbezi wala Sinza,” alisema Uwoya kwa masikitiko.


Akaendelea kueleza kuwa, kufuatia hali hiyo alianza kuwasiliana na Ndikumana ili kujua aliko lakini matokeo yake aliambulia meseji za vitisho.


“Nilipojaribu kumtafuta kupitia simu yake ili kujua aliko alianza kunitumia meseji za vitisho tena mbaya zaidi vilikuwa vitisho juu ya mtoto, kwa kweli amenichanganya sana.”


“Hata kama tunagombana mara kwa mara lakini kitendo cha kutoroka na mtoto kisha kunitumia meseji za vitisho siyo sahihi na kwa kweli siwezi kukivumilia, nimempa saa 24 amrudishe mtoto laa sivyo nitamchukulia hatua za kisheria,” alisema Uwoya.

 Tangu siku hiyo Uwoya alikuwa katika jitihada za kufungua jalada la kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Posted by Bigie on 12:45 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.