PENZI LA H. BABA NA FROLA LASAMBARATIKA......

Hatimaye penzi lililokuwa hot kwa takribani mwaka mmoja kati ya Flora Festo Mvungi ‘The One’ na Hamis Ramadhan Baba ‘H.Baba’,  limevunjika.

Habari za kuaminika zilizagaa mtaani  mwishoni mwa wiki iliyopita. Flora alidaiwa kushindwa na nyumba ya H.Baba iliyopo maeneo ya Kijitonyama, Dar es Salaam hivyo akarejea nyumbani kwa mama yake aishie Kimara, Dar.

 Habari hizo zilidai kuwa Eti kisa Flora amechoka kuishi na H.Baba na kwamba anahitaji uhuru zaidi.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, mpekuzi wetu aliwatafuta wawili hao ili kujiridhisha na data ambapo kwa nyakati tofauti, walikiri kumwagana laivu.

Flora: “Nimeachana na H.Baba ili ajue nimekasirika, ni kweli nimeondoka, niko nyumbani kwetu, siwezi kuacha kazi yangu ya sanaa na ielewke kwamba sijachoka, lakini nahitaji uhuru.”

H.Baba: “Duh! Nani kawaambia? Ilaaa…aaah, ni kweli kuna tofauti ndogo, lakini naamini atarudi muda si mrefu kwani bado tunapendana.”

Posted by Bigie on 12:45 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.