VITOTO VYA BONGO FLEVA VYAMPONZA REHEMA FABIAN......
JAMII 12:59 AM
Rehema Fabian, amekula kichapo kutoka kwa mchumba’ke mtarajiwa ambaye ni pedeshee maarufu jijini Dar es Salaam maarufu kwa jina la Jacob The Best, kufuatia skendo ya kujilegeza kwa Msanii chipukizi wa Bongo Flava.
Rehema ambaye ni mshiriki wa Miss Kiswahili 2009, aliweka wazi mbele ya Mpekuzi wetu kuwa alipata kibano kutoka kwa jamaa huyo hivi karibuni walipokuwa kwenye kiwanja cha wastaarabu cha Nyumbani Lounge, Dar.
Rehema anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva alikutwa na sheshe hilo baada ya kuonekana kwenye gazeti moja akiwa kihasara na chipukizi wa muziki wa Kizazi Kipya.
Alidai kuwa alijuta kuzaliwa kwani alipewa vitasa vya kutosha na jamaa huyo huku akiomba msamaha na kuahidi kutorudia kutokana na maumivu aliyoambulia.
“Nimejuta kuwa karibu na maandagraundi, naahidi sitarudia na namuomba mchumba’ngu asahau yaliyopita tugange yajayo.”