WATOTO WA MAREHEMU MEJA ALEX G. NYIRENDA WAPANDA MLIMA KILIMANJARO KUMKUMBUKA SHUJAA HUYO
JAMII 5:48 PM
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kanali Mstaafu Ameen Kashmiri wakati wa sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wiki iliyopita, ambapo alimmwagia sifa mwanajeshi huyu mstaafu kwa kuwa mmoja wa mashujaa wachache wa Uhuru walio hai hadi sasa. Kanali Kashmiri ndiye aliyebeba bendera ya Tanganyika huru siku ile hapo hapo uwanja wa Uhuru wakati Tanganyika inapata Uhuru na bendera yake kupandishwa.
![]() |
| Mwalimu Nyerere akijiandaa kuishusha bendera ya mkoloni na kupokea ya Tanganyika huru iliyobebwa na Kanali Ameen Kashmiri (kushoto) usiku huo wa uhuru miaka 50 iliyopita |

Watoto wa Marehemu Brigedia Alex Gwebe Nyirenda,Tima pamoja na kaka yake Alex wakiwa wameshika koti ambalo baba yao alilivaa wakati alipopanda Mlima Kilimanjaro na kuweka Mwenge wa uhuru pamoja na bendera ya Taifa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro Nchi yetu ilipopata Uhuru mwaka 1961.
Alex ameshika Mwenge ambao nao pia watauwasha na kuuweka kileleni huko siku ya Desemba 9, 2011 ikiwa kama heshima na kumbukumbu ya kazi aliyoifanya marehemu baba yao miaka 50 iliyopita.
Kwa mujibu wa Suzyo Gwebe-Nyirenda, binti wa Brigedia Nyirenda, tukio hilo, linaloenda kwa jina la GWEBE-NYIRENDA MEMORIAL KILIMANJARO EXPEDITION, litafanyika kila mwaka na kwamba mwakani hata wajukuu watashiriki pamoja na wadau wataopenda kujiunga katika msafara huo. Suzyo Gwebe-Nyirenda hakuweza kushiriki kutokana na kupata ajali ya gari, na hali yake inaendelea vyema. Kitindamimba wao, Tiwonge Gwebe-Nyirenda hakuweza kuja kutoka Lusaka, Zambia, aliko kikazi kwa sababu zisizozuilika.
Alex ameshika Mwenge ambao nao pia watauwasha na kuuweka kileleni huko siku ya Desemba 9, 2011 ikiwa kama heshima na kumbukumbu ya kazi aliyoifanya marehemu baba yao miaka 50 iliyopita.
Kwa mujibu wa Suzyo Gwebe-Nyirenda, binti wa Brigedia Nyirenda, tukio hilo, linaloenda kwa jina la GWEBE-NYIRENDA MEMORIAL KILIMANJARO EXPEDITION, litafanyika kila mwaka na kwamba mwakani hata wajukuu watashiriki pamoja na wadau wataopenda kujiunga katika msafara huo. Suzyo Gwebe-Nyirenda hakuweza kushiriki kutokana na kupata ajali ya gari, na hali yake inaendelea vyema. Kitindamimba wao, Tiwonge Gwebe-Nyirenda hakuweza kuja kutoka Lusaka, Zambia, aliko kikazi kwa sababu zisizozuilika.

Watoto wa Nyirenda akiwa anajiandaaa kupanda Mlima Kilimanjaro huku kaka yake akimsubiria.

Watoto wa Marehemu Mzee Alex Nyirenda,Alex Foti Gwebe Nyirenda akiwa na mdogo wake Tima Gwebe Nyirenda wakiwa wameshasaini kwenye geti la kuingilia na kupata kibali wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
![]() | |
| Juu na chini ni watoto na marafiki wa Mzee Nyirenda wakipata semina ya namna ya kukwea mlima Kilimanjaro kabla ya safari kuanza |

Watoto wa Marehemu Mzee Nyirenda,Alex pamoja na nduguye Tima wakiwa pamoja na watu walioongozana nao wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa hoteli ya Marangu,Desmond Brice -Bennnett wakati alipokuwa akiwapa maelekezo kuhusu sheria za mlima kilimanjaro pamoja na njia ambazo watapita
![]() |
| Picha ya pamoja kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro. Wapandaji hao ni pamoja na Kanali mstaafu Ameen Kashmiri (wa nne toka kushoto) ambaye ndiye aliyekuwa mmoja wa maafisa wa jeshi katika kikosi cha bendera usiku wa manane wakati Tanganyika inapata Uhuru wake. Wengine ni Mobeen Kashmiri, Paul Mason, Aunali Rajabali, Lorley Lavilla, Mohamed Khimji, Tima Gwebe-Nyirenda Kuwani na Alex Foti Gwebe-Nyirenda. Meja Kashmiri, ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Meja Nyirenda, ndiye baba mlezi wa familia hiyo ya rafikiye kipenzi |



At the eve of Tanzania's independence, Brig. Nyirenda hoisted Tanzania's flag (then Tanganyika) and placed the Uhuru Torch on the summit of Mt. Kilimanjaro as the Union Jack was lowered at the National Stadium in Dar es Salaam at the same time.
Two years earlier, former President Julius K. Nyerere, in a speech to the Tanganyika Legislative Assembly, said the following:
"We the people of Tanganyika, would like to light a candle and put it on top of Mount Kilimanjaro which would shine beyond our borders giving hope where there was despair, love where there was hate, and dignity where there was before only humiliation...."
That candle (which came to be known to Tanzanians as the Uhuru torch) was placed on Mt. Kilimanjaro by Lt. Nyirenda, and signalled Tanzania's long and unwavering commitment to the liberation struggle of those African countries that remained in the early sixties under colonialism and white minority rule.
Brig. Nyirenda was the first Tanganyikan in 1958 to graduate from Sandhurst Military Academy in England. He also became, prior to independence, the first African to become an officer in the King's African Rifles.
He was also related, through a common ancestor, to former Zambian President, Dr. Kenneth Kaunda, which is a stark reminder to Africans that they are often closer to each other than artificial boundaries would indicate.



