DAVINA AKERWA NA MICHIRIZI ILIYOKO MAPAJANI MWAKE
JAMII 11:38 PM
MSANII za wa filamu Bongo, Halima Yahya Mpinge ‘Davina’ anakerwa na michirizi aliyonayo mapajani na kumfanya ashindwe kuvaa nguo fupi kama wavaavyo wasanii wenzake.
Akizungumza na mpekuzi wetu juzikati jijini Dar, Davina alisema ili kuificha michirizi hiyo analazimika kuvaa nguo ndefu licha ya kwamba hapendi.
“Natamani sana kuvaa nguo fupi kama wasichana wenzangu lakini siwezi kutokana na michirizi niliyonayo mapajani. Nikilazimisha kuvaa nguo fupi huwa naonekana kama kituko kila ninapopita,” alisema Davina.