AISHA BUI AKERWA NA UKUBWA WA MATITI YAKE....
JAMII 11:33 PM
Staa wa sinema za Bongo, Aisha Bui amesema anakerwa sana na ukubwa wa matiti yake kiasi kwamba, anafikiria jinsi ya kuyapunguza
Akizungumza na mpekuzi wetu hivi karibuni , Aisha alisema kuwa Matiti hayo yanamkera sana mpaka amefikia hatua ya kufanya mikakati ya kuyafanyia upasuaji.
“Kwa kweli nakerwa sana na haya matiti yangu, ni makubwa mno. Hapa nilipo nina mipango yangu ya kifedha ikikamilika nitakwenda hospitali kuyafanyia upasuaji kwa maana ni kero sasa,” alisema Aisha.
Msanii huyo aliongeza kuwa mbaya zaidi matiti yake yalivyo makubwa yanamfanya ashindwe kupendeza anapovaa nguo hata kama ni za thamani kiasi gani.
“Unajua kutokana na ukubwa wa matiti yangu hata nguo nikivaa hazinipendezi kama ambavyo ningekuwa na matiti madogo,” alifunguka Aisha.