HAMAD RASHID MOHAMED NA WAJUMBE WENGINE WATATU WATIMULIWA UANACHAMA CUF
JAMII 2:17 PM
Akitangaza uamuzi huo katika Hoteli ya Manson Mji Mkongwe jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema mbali na Hamad Rashid, pia baraza hilo limewavua uanachama wajumbe wengine watatu wa Baraza Kuu.
Wajumbe hao ni Doyo Hassan Doyo kutoka katika Mkoa wa Tanga, Juma Sanani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na Shoka Khamis Juma, aliyewahi kuwa Mbunge wa Micheweni kwa tiketi ya CUF.
“Baraza Kuu la CUF limewafukuza viongozi hao baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili kutoka wajumbe wa Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka wajumbe Zanzibar,” alisema Mtatiro.
Mjumbe mwingine: Yasin Mrotwa amepewa onyo kali na karipio. Kwa mujibu wa Mtatiro, yeye pia anaendelea kuchunguzwa na Baraza Kuu.
“Sisi tumeweka pingamizi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa mkutano wa Baraza Kuu na hati ya Mahakama ipo wanayo...sasa nawashangaa wanakiuka sijui kwa nini?” Alihoji Hamad Rashid.