UDOM WAMALIZA MGOMO SHINIKIZI WA KUDAI FEDHA ZA KUJIKIMU




WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kitengo cha Elimu (Collage of Education) ambao
juzi waligoma kushinikiza kupatiwa fedha za kujikimu, jana walimaliza mgomo na kurejea madarasani.

Wanafunzi hao waligoma kwa lengo la kushinikiza uongozi kuwapatia fedha za kujikimu kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB).

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa harakati za kudai fedha za kujikimu, Rafiki Rufungo wameamua kurejea madarasani baada ya kuahidiwa kulipwa fedha hizo Ijumaa.

“Mgomo umesitishwa, tunasubiri Ijumaa ya wiki hii kulipwa fedha zetu kama tulivyoahidiwa na chuo,” alisema Rufungo.

Awali, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alithibitisha kuwa wanafunzi hao watalipwa kama walivyoahidiwa kwa kuwa tayari fedha zao zipo. 


Katika kuthibitisha hili,kiongozi mmoja wa serikali ya wanafunzi toka chuo cha sanaa, jana aliandika katika mtandao wa facebook kuwa tayari cheque  zimekwisha pelekwa bank kwa ajili ya malipo ya wanafunzi hao



Wakati huo huo, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St John nao walianza masomo baada ya chuo hicho kufungwa kwa muda kutokana na vurugu za kudai kupatiwa fedha za kujikimu.

Ofisa Uhusiano na Msemaji wa chuo hicho, Karim Meshack alisema kuwa kazi ya kujisajili imekamilika juzi jioni na wanafunzi wameingia madarasani jana kuendelea na masomo.

“Wanafunzi wamemaliza kazi ya kujisajili juzi jioni na hali iko shwari kabisa, wameingia madarasani wanaendelea na masomo kama kawaida,” alisema Meshack

Posted by Bigie on 2:00 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.