KIONGOZI WA KUNDI LA KIGAIDI LA BOKO HARAM AWATOROKA POLISI IKIWA NI MASAAA 24 TANGU AKAMATWE


IDARA ya polisi nchini Nigeria, imethibitisha kuwa mshukiwa mmoja ambaye anaaminika kuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram, ametoweka, baada ya wapiaganaji wa kundi hilo kushambulia msafara wa polisi ambao ulikuwa ukimpeleka kizuizini.

Mshukiwa huyo alikuwa amekamatwa na polisi siku ya Jumamosi na alikuwa akisafirishwa korokoroni ili kuwapa maafisa wa polisi nafasi ya kufanya uchunguzi zaidi.

Baada ya kukamatwa mshukiwa huyo alikabidhiwa kamishna wa polisi, ambaye aliamrisha mshukiwa huyo apelekwe katika kituo kimoja cha siri cha Abaji.

Wakati msafara huo ulipokuwa njiani, wapiganaji wa kundi hilo waliushambulia na kumkomboa kiongozi huyo wa Boko Haram.

Idara ya polisi nchini humo, imesema maafisa wake kadhaa hawakuwajibika na serikali ya nchi hiyo imemsimamisha kazi kwa muda kamishna huyo wa polisi.

Ikiwa uchunguzi utabainisha kuwa yeye na maafisa wake walihusika na kutoweka kwa mshukiwa huyo, huenda wakafunguliwa mashtaka ya uhalifu.

Kile ambacho polisi hawajataja ni kwamba mshukiwa huyo, kwa jina Kabir Sokoto, alikamatwa akiwa ameandamana na mwanajeshi katika chumba kimoja cha Gavana wa jimbo la Bornu kilichoko Abuja wikendi iliyopita.

Maafisa wa serikali wa jimbo hilo mjini Maiduguri walithibitisha kukamatwa kwa mshukiwa huyo.

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimetangaza kwamba mshukiwa huyo ni afisa wa ngazi ya juu na ndiye anayeaminika kuwa naibu wa kiongozi wa kundi hilo la Boko Haram .

Posted by Bigie on 6:52 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.