JACK PENTEZEL ("JACK WA CHUZ") ASUSA CHAKULA MSIBANI KISA HAKIKUWA NA NYAMA


MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Jack Pentezel ‘Jack wa Chuz’ juzi kati aliushangaza umati uliofurika kwenye msiba wa mkongwe wa sanaa ya maigizo Bongo, Fundi Said ‘Mzee Kipara’ baada ya kususa sahani ya chakula iliyokosa mboga.

Jack alifanya kituko hicho kwenye shughuli hiyo ya mazishi iliyofanyika Alhamisi iliyopita Kigogo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati wa watu wakiwemo wasanii wa filamu, wanamuziki na viongozi wa serikali.

Katika tukio hilo, Jack alinawishwa mikono na kupewa sahani iliyosheheni pilau lakini alipotaka kuanza kula aligundua hakukuwa na nyama ndipo alimuuliza muandazi huyo kwa nini pilau halikuwa na nyama lakini kabla ya majibizano zaidi  Jack alimtaka muandazi huyo kuondoka na chakula chake.

Mpekuzi wetu alipotaka kuzungumza na msanii huyo kuhusiana na tukio hilo alimtaka aachane na ishu hiyo.

Posted by Bigie on 6:54 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.