WANAFUNZI WA KIISLAM JANA WALIANDAMANA JIJINI DAR KUPINGA KUFUKUZWA SHULE WANAFUNZI WENZAO 20
Posted by Bigie
JAMII
7:37 PM
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi waislamu waliofanya maandamano ya amani na kukusanyika katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana kupinga Uongozi wa Shule ya Sekondari Ndanda kuwafukuza wanafunzi 20 wa kiislamu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akiwasili katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana kuzungumza na wanafunzi wa kiislam waliokuwa wameandamana jana kupinga Uongozi wa Shule ya Sekondari Ndanda kuwafukuza wanafunzi 20 wa kiislamu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo. Rais wa Wanafunzi wa kiislamui, Jafari Mneto akizungumza katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam baada ya Wanafunzi wa Kiislamu kufanya maandamano ya amani. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleima Kova akiagana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa mara baada ya kuzungumza na wanafunzi wa Kiislamu.

Posted by Bigie
on 7:37 PM.
Filed under
JAMII
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0