MTANGAZAJI MAARUFU WA RADIO TIMES FM "DIDA" AZUSHIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

MTANGAZAJI  wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, amezushiwa tena skendo ya kwamba eti anauza madawa ya kulevya.

Akizungumza kwa masikitiko juu ya uzushi huo, Dida alisema ameshangaa kuona mtu mmoja ambaye hamjui akisambaza ujumbe mtandaoni kuwa eti anafanya biashara hiyo haramu na ndiyo maana kila siku anakwenda mamtoni.

Ujumbe huo ulitumwa kwenye ukurasa wa Dida wa Facebook na kwenye blog yake hivyo kufanya watu walioutembelea kushangazwa na maneno hayo.

Hata hivyo, Dida alimjibu aliyeposti maneno hayo ya uzushi kwa kusema: “Kwa ufupi wewe mdau usiyependa maendeleo yangu, mimi ni Dida na nitabaki kuwa Dida labda Mungu apangue.

“Kama hicho unachokisema unaona ni dili jaribu na wewe tuone, utabakia manenomaneno mtoto kutoka Tanga ndiyo kwanza napeta….”

Posted by Bigie on 7:28 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.