Bondia wa kike,Lulu Kayege ajifua kwa ajili ya kuwakabiri wapinzani wake
habari za kitaifa 9:11 AM
Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala, Kondo Nassoro, akimfundisha bondia chipkizi wa kike, Lulu Kayege, wa Dar es salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kumi bora yatakayofanyika june 15 katika ukumbi wa Panandi Ilala Bungoni jijini. Bondia huyo amesema kuwa anauhakika wa kuwachapa wapinzani wake watakaojitokeza kuomba 'Gem' na yeye kutokana na maandalizi kabambe na kujiamini katika mchezo huo. ''Nimekuja kuleta mabadiliko katika mchezo wa ngumi kwa upande wa wanawake kwani naupenda mchezo huu kutoka moyoni na naamini nitaweza kufanya vizuri kwani nimekuwa nikifuatilia sana mapambano ya wanawake wenzangu na kuona mapungufu yao ambayo mimi nitayatumia kama chalenge kwangu ili niweze kuwa tofauti ya wao'' alisema LULU. Picha na Super D