MATUKIO MBALI MBALI KATIKA ZIARA YA NAIBU SPIKA, JOB NDUGAI NCHINI KOREA KUSINI
habari za kitaifa 11:24 AM
Mwakilishi wa heshima wa Tanzania, Balozi Johan ambae aliwahi pia kuwa Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini akimpa maelezo Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai wakati alipomtembeza katika jengo lenye historia ya waliowahi kuwa wafalme wa Korea. Nchi hiyo iliamua kuondokana na utawala wa kifalme na kuwa Jamhuri. Mwaka 2012 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Desemba.
Mhe. Naibu Spika Job Ndugai akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu vyakula vya asili vya watu wa Korea wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yake na Balozi Johan. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea, Bi. Hahn. Wa kwanza kulia ni Ndugu Athuman Kwikima, Afisa Tawala katika Ofisi ya Bunge alieko masomoni katika Chuo Kikuu cha Seoul nchini humo.
Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai akiwa katika mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Korea Kusini alipokutana nao muda mfupi kabla ya kukutana na Watanzania waishio nchini humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Korea Kusini, Bw. Msofu akimkabidhi Mhe. Naibu Spika risala ya wanajumuiya hao ili aweze kuifanyia kazi mara baada ya kuisoma mbele yake.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Judith anaesoma nchini Korea akimuuliza swali Mhe. Naibu Spika Job Ndugai mara baada ya Naibu Spika huyo kuwahutubia watanzania waishio nchini Korea. Mhe. Naibu Spika alihitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki.PICHA ZOTE NA SAIDI YAKUBU WA OFISI YA BUNGE.