MWAKYEMBE AWAFUKUZA KAZI VIGOGO WA SHIRIKA LA NDEGE LA ATCL


Barua iliyotolewa na kutiwa saini leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omar Chambo ikiwa na TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, inasema:

Yah. KUSITISHWA KWA NYADHIFA ZA WATUMISHI WA KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA (ATCL)

Bw. Paul T. Chizi aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) tarehe 06/08/2011. Hata hivyo, utaratibu wa uteuzi wake haukufata Sheri, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Hivyo, kupitia sheria Na. 8 ya mwaka 2002 na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 Na. 17(4), Mheshimiwa Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb.), Warizi wa Uchukuzi, ametengua Uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania kuanzia 5 Juni 20112. Kanuni hii inaelzea bayana kuwa kama mtumishi atakuwa ameteuliwa kwa kukiuka kifungu cha 17(1) au (3) za Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, itakuwa ni Mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wa utumishi wake mara moja.

Ili kazi ziweze kuendelea, Mheshimiwa Waziri amemteua Kapteni Lusajo M. Lazaro kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL kuanzia tarehe 05 Juni, 2012.

Aisha, Mhesimiwa Waziri wa Uchukuzi amewasimamisha kazi watumishi wafuatao:

         (i)    John Ringo – Kaimu Mkurugenzi na Uhandisi

        (ii)    Amini N. Mziray – Mwanasheria wa ATCL

        (iii)   Justus Bashara – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha

       (iv)   Josephat Kagirwa – Kaimu Mkurugenzi wa Biashara

Posted by Bigie on 9:23 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.