"HAKUNA HAJA YA KUPOTEZA MUDA UKIJIKOSHA KWA MPENZI WAKO WA ZAMANI MAANA KUACHANA NI MAAMUZI NA SIYO HISIA"....SIZE 8



Kumekuwa na mjadala mkali sana  juu  ya  kurudiana kwa wapenzi walioachana.Mjadala  huu  umevuta hisia za wengi na kumfanya  Msanii  size 8  naye  aeleze ya moyoni......

Kwa mujibu wa size 8, kujirudi kwa mpenzi wako uliyeachana naye ni kosa kubwa sana  na  ni maamuzi ambayo si sahihi.......

Yeye anaamini kuwa  kuachana  ni Maamuzi  na siyo Hisiana Maamuzi hayo ni lazima yaangaliwe kwa kina zaidi.

"Kuachana  ni maamuzi na siyo hisia.Lazima ujiulize kwa kina kwanza, je ni kwa nini mlifikia hatua mkaachana. Inawezekana wakati huo mwenzio alikuwa na mtu na hivyo kukuona hufai.
Ameenda huko katumika weeee!!!!...baada ya kuchoka sasa  anataka mrudiane huku akikudanganya kwa maneno mazuri eti aliondoka kimakosa  au aliondoka na mwili, roho bado iko na wewe.
Huo ni uongo.Na hii ndo sababu inayonifanya niamini kuwa mkitengana hakuna kurudiana kwa sababu angekuwa anakupenda naturally  basi angevumila  na asingekuwa tayari kukuona  ukiteseka na maumivu ya mapenzi"Alieleza Size 8 na kuongeza kuwa :

"Sina maana muwe maadui.ila zingatieni faragha na mipaka yenu.Msije mkajikuta mnafanya mapenzi ya maigizo.Kama ni salamu basi salam tu na si vinginevyo"


Posted by Bigie on 5:56 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.