JACK WOLPER AJIPANGA KUTOKA NA" AFTER DEATH " YENYE LENGO LA KUMUENZI KANUMBA
BONGO MOVIE, habari za kitaifa, Jackline Wolper 4:10 AM
Muigizaji wa kike wa Bongo Movies Jackline Wolper yupo location kushoot filamu yake mpya iitwayo ‘After Death’ anayoigiza na watoto wawili waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba kwenye filamu zake za ‘Uncle JJ’ na ‘This is It’ Jennifer na Patrick.
Amesema baada ya kifo cha Kanumba, aliwaahidi watoto hao kuwa ataendeleza vipaji vyao vya uigizaji kwakuwa Kanumba alikuwa kama baba yao.
Jackline amesema After Death itashirikisha wasanii wengine kama Shamsa Ford, Mariam, Pancho Mwamba na wengine.
Ameongeza kuwa kwenye filamu hiyo amemtumia mtu ambaye anafanana sana na Kanumba ili kuifanya story iendane naye.