TAFF YAPANGA KUWAANGAMIZA WANAUME WAPENDA NGONO


KIMENUKA,  kwa wasanii wapenda ngono kwani Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), chini ya Rais wake Simon Mwakifwamba limesema kuwa litawasaka wasanii wa kiume wapenda ngono.

 Hali hiyo imekuja kufuatia skendo ya baadhi ya waandaaji wa kiume kudaiwa kuwanyanyasa wasanii wa kike kwa kuwataka kimapenzi ili  kuwapa nafasi ya kuigiza.

Akizungumza na mwandishi wetu , Mwakifwamba alisema anaandaa siku maalum kwa ajili ya kuzungumza na waandaaji hao baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasanii wa kike hivi karibuni Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

“Kama Rais wa Taff nimepokea malalamiko yao na ninayafanyia kazi,  nitazungumza nao maana hata mimi mwenyewe imeniuma na ninaona wasanii wa kike wanahitaji msaada zaidi,” alisema Mwakifwamba.

Baadhi ya wadau walisema kama Taff itachukua hatua hiyo, Bongo Movie hali itakuwa ni tete kwa wasanii hasa wa kiume.

Posted by Bigie on 1:04 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.