BREAKING NEWS: SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

                                   

MSANII WA VICHEKESHO NA MUZKI SHARO MILIONEA  AMEFARIKI LEO HUKO MUHEZA TANGA KWA AJALI YA GARI AMBAPO NDUGU YAKE WA KARIBU SNURA MUSHI AMETHIBITISHA  TUKIO HILO  KWA NJIA YA SIMU .....

 

Naye Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha  kutokea kwa  kifo cha  wa Sharobaro, kufuatia  ajali ya gari  katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga  ambako ndio nyumbani kwao.......

 

MPAKA SASA MWILI UPO  HOSPITALI TEULE   YA MUHEZA ,TANGA

           


Mpekuzi imepokea habari hizi kwa mstuko na masikitiko makubwa kwani nyota ya Sharo Milionea ndiyo ilikuwa inaanza kung'ara katika anga za muziki pamoja na matangazo ya biashara, akiwa kayapumulia pumzi mpya wa ubunifu na weledi katika kupeleka ujumbe kwa watazamaji ambao wakubwa na wadogo walimpenda.

Mola aiweke roho ya marehemu 
mahali pema peponi - Amina
TUTAZIDI  KUTOA  UPDATE:

Posted by Bigie on 11:51 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.