VIBAKA WALIKATA KIDOLE CHA SHARO MILIONEA NA KUTAMBAA NACHO.....
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 7:40 AMSharomilionea.
Siku kadhaa baada ya marehemu msanii sharomilionea kuzikwa, vile vitu ambavyo vilisemekana kupotea ama kuibiwa wakati wa ajali vimeanza kupatikana. Akithibitisha habari za kupatikana kwa vitu hiuvyo, swahiba wake wa karibu ambaye alikuwa akiishi na Sharomilionea Kitale amesema amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kule Muheza Tanga kwamba baadhi ya vitu vimepatikana.
Kwa mujibu wa maelezo yake, vitu ambavyo vilikuwa vimeibwa ni pamoja nasimu mbili aina ya Blackberry na Samsung, Viatu, Cheni, tairi la spea ya gari, Betri, Radio ya gari na shilingi milioni sita taslimu ambazo alikuwa akimpelekea mama yake.
Bwana kitale aliendelea kwa kusema, cha kusikitisha zaidi katika tukio hilo la wizi, ni unyama uliofanywa na wezi hao ambapo baada ya kushindwa kumvua pete kwenye kidole cha msanii huyo, waliamua kumkata kidole na kuondoka na pete hiyo.
Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizonazo kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji kuna wanakijiji wamerudisha baadhi ya vitu kama Simu ya Mkononi,Pete,Cheni, Jeans, T-shirt,Viatu, ambapo walisema wamerudisha baada ya kugunduliwa na wanakijiji wenzao ambao walitoa taarifa baada ya kugundua vitu walivyokuwa navyo ni mali ya marehemu msanii Sharomilionea.
Kitale alisema “kuna kijana mmoja anayeitwa David ambae ni ndugu na mwenyekiti na wenzake ambao walitajwa na wanakijiji wenzao kwa kuhusika yeye pamoja na wenzake kufanya kitendo hicho ya bila kujua wanao mfanyia alikuwa ni Sharro baada ya kutambua watu hao wakafanya ionekane vitu hivyo vimepatikana kutoka kwa wanakijiji."
Kitale alimalizia kwa kusema kwa sasa vitu ambavyo havijapatikana ni pamoja na Betri, Tairi la spea, Radio ya gari na pesa ambazo anasema suala hilo tayari lipo poilisi kwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo habari zilizotufikia zinadai kuwa Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma hizo za za kumkata vidole na kumuibia marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya gari
MSAKO KALI WA POLISI MKOANI TANGA WAFANIKISHA UPATIKANI WA BAADHI YA VITU VYA SHARO MILIONEA VILIVYOKUWA VIMEIBIWA
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 12:48 AMWatu wasio na huruma walishindwa kutoa msaada kwa marehemu sharomilionea katika kumuokoa na kuona ni bora vitu alivyokua navyo wavichukue .....
Lakini uchunguzi wa polisi kwa kushirikiaana na wananchi na umeweza kupitisha msako mkali baadhi ya vitu vilivyochukuliwa katika tukio hilo vimepatikana.
AKIONGEA kwa njia ya simu na blog hii, aliekua rafiki wa karibu wa sharo milionea KITALE amevitaja vitu vya marehemu vilivyopatikana ni pamoja na SPEAR TYERE,RADIO YA GARI,BETRI YA GARI,SAA YA MKONONI,na pia kwa masaada ya jeshi la polisi uliweza kusaidia kupatikana kwa simu yake ya mkononi ya SHAROMILIONEA huku vitu vingine ikwemo SURUALI AINA YA JINSI NA T-SHIRT YAKE BADO HAVIJAWEZA KUPATIKANA na polisi jijini tanga wanaendelea na msako wa kuvikamata vitu vingine vilivyopotea katika eneno la tukio
WAOMBOLEZAJI WALIOZIMIA WAKATI WA MAZISHI YA SHARO MILIONEA JANA MKOANI TANGA PAMOJA NA VIDEO YA RIPOTI YA ITV
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 6:23 AMSAFARI YA MWISHO YA SHARO MILIONEA MCHANA HUU....
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 2:51 AM



Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele



Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.
MAMIA WASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA SHARO MILIONE MCHANA HUU
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 2:40 AMTASWIRA MBALIMBALI ZA GARI ALILOPATA NALO AJALI MSANII SHARO MILIONEA NA JINSI UMATI WA WANANCHI ULIVYOFURIKA NJE YA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI TEULE YA MUHEZA
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 6:52 PMGari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Baadhi ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni .
Wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari.
WASANII WATOA NYIMBO MBILI ZA HUZUNI SANA WAKIMLILIA MSANII SHARO MILIONEA....
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 9:28 AMDOWNLOAD WIMBO HUU WA MAOMBOLEZO
Tunda Man ft. Mirror & Raymond - R.I.P Sharomilioner
Huu ni wimbo ambao kiukweli umenitoa machozi
---------------------------------------------------------------------
Huu chini ni Wimbo ambao umefanywa na producer monagangstar....
Waliofanya hii ngoma ni DOGO JANJA,PNC KUTOKA MTANASHATI/.OSTAZ JUMA NAMUSOMA) ,STAMINA,COUNTRY BOY MTU CHEE,NAY WA MITEGO,SAPRANO,SUMA MNAZALETI,ELLY NIZO,BRIGHT,MAKOMANDO WAZEE WA KIBEGA,N,K
DOWNLOAD WIMBO HUU.NI WIMBO WA MAOMBOLEZO
*
HIKI NDO CHANZO CHA AJALI YA SHARO MILIONEA PAMOJA NA SIKU KAMILI YA MAZISHI
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 6:40 AM Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.
Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.
Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi.
Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.
Kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na mwili wa marehemu katika eneo la tukio,ndipo mama mmoja aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na kuharibika vibaya.
Mganga mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo hapo.
Hata hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi kituo cha polisi wilayani humo.
Mwili wa Sharo utazikwa kesho jioni .
CHAT YA MWISHO YA SHARO MILONEA NA LINEX WAKIONGELEA MAMBO YA BARABARANI....
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 1:29 AMAUDIO: KAMANDA WA POLISI TANGA ATOA UFAFANUZI KUHUSU KIFO CHA SHARO MILIONEA
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 1:46 PMNamkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
BREAKING NEWS: SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI
Posted by Bigie habari za kitaifa, SHARO MILIONEA 11:51 AMMSANII WA VICHEKESHO NA MUZKI SHARO MILIONEA AMEFARIKI LEO HUKO MUHEZA TANGA KWA AJALI YA GARI AMBAPO NDUGU YAKE WA KARIBU SNURA MUSHI AMETHIBITISHA TUKIO HILO KWA NJIA YA SIMU .....
Naye Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha kutokea kwa kifo cha wa Sharobaro, kufuatia ajali ya gari katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga ambako ndio nyumbani kwao.......
MPAKA SASA MWILI UPO HOSPITALI TEULE YA MUHEZA ,TANGA
Mpekuzi imepokea habari hizi kwa mstuko na masikitiko makubwa kwani nyota ya Sharo Milionea ndiyo ilikuwa inaanza kung'ara katika anga za muziki pamoja na matangazo ya biashara, akiwa kayapumulia pumzi mpya wa ubunifu na weledi katika kupeleka ujumbe kwa watazamaji ambao wakubwa na wadogo walimpenda.
Mola aiweke roho ya marehemu
mahali pema peponi - Amina
TUTAZIDI KUTOA UPDATE:
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

















