JE WEWE NI MSANII NA HUZIJUI HAKI ZAKO???......UNGANA NA MDAU JOHN KITIME AKUFUNGUE MACHO
habari za kitaifa 10:34 AM
Mahojiano haya na Ndg John F Kitime yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na vipaji hapa nchini.
Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali mapato.
Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni
pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali,
utekelezaji wa hatua hii utaanza rasmi tarehe 1 Januari,
2013.
Mahojiano haya yanaangalia uelewa wa wadau mbalimbali kuhusiana na mabadiliko ya sheria hii,nini mawazo ya wadau ya nini kifanyike ili kuweza kuweka taratibu nzuri za kusaidia utekelezajji wa sheria husika
Msikilize vyema John F Kitime uweze kufahamu vyema yale anayoyajuwa na anayodhani ni muhimu kuwa sawa katika mabadiliko ya sheria hii!:-
<<<http://youtu.be/A2jRIqoqE_I>>>
Wasalaam.
E.N.M.Manase
Mdau -TFCA
AU MSIKILIZE HAPO CHINI KWA KUBOFYA "PLAY"
Posted by Bigie
on 10:34 AM.
Filed under
habari za kitaifa
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0