LIVE VIDEO YA BARNABA NA SUMA LEE WALIVYOPAGAWISHA HUKO UK


Urban Pulse Creative inawaletea video fupi ya show iliyofanyika London ikiwajumuisha wasanii Barnaba na Suma Lee tarehe 22.12.12

Barnaba akiimba kwa hisia.
Hakunaga kama Suma Lee 

Kassu Ent iliandaa tamasha maalum kutoka kwa wasanii wetu wa kizazi kipya iliowajumuisha Barbaba na Suma Lee. Tamasha hili lilikwenda sambamba kwa kusherekea miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya jumamosi tarehe 22.12.12 jijini London katika ukumbi wa Stratford.

Mgeni rasmi alikua naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na mkewe Irene Kilumanga. 
Aidha Mh Balozi Kilumanga aliwapongeza watanzania walioweza kuja kujumuika na kusherekea pamoja katika siku hii na kuwasihi kuendeleza mshikamano kwa kuishi pamoja kwa amani na upendo.
Suma Lee akifanya vitu vyake.


Barnaba akiwadatisha mashabiki na Magume gume. 

HII  NDO LIVE VIDEO YA  HIYO  SHOW

Posted by Bigie on 7:47 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.