"RAY HAYAJUI MAUMBILE YANGU NA SINA UHUSIANO NAYE".....JOHARI
BONGO MOVIE, habari za kitaifa, JOHARI 11:41 PM
MSANII wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa, licha ya watu kudai kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’, anaapa hawajawahi kufikia hatua hiyo.
“Naapa sijawahi kulala na Ray. Nashangaa hizi habari zinavyozidi kuenea. Kwa hilo niko tayari kushika hata Biblia kuapia kuwa sina na wala sijawahi kuwa na uhusiano na Ray, uhusiano wetu ni wa kikazi tu,” alisema Johari.
Johari kwa muda mrefu amekuwa akidaiwa kutoka na Ray kwa siri lakini mwenyewe anakana huku wadau wakizidi kushikilia kuwa habari hizo zina ukweli ndani yake.
Posted by Bigie
on 11:41 PM.
Filed under
BONGO MOVIE,
habari za kitaifa,
JOHARI
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0