SIKUKUU YA KRISMAS YAMFANYA DEO FILIKUNJOMBE ( MBUNGE ) AMWAGE MACHOZI...


Mbunge wa jimbo la Ludewa na familia yake wakiwajulia hali wagonjwa kama ilivyoutaratibu wake wa kila sikukuu kula na wagonjwa wa zanahati na Hospitali mbalimbali jimboni mwake.
Picture
Mbunge Filikunjombe akitazama mikoni ya mtoto Diana ambayo imeungua kwa moto kushoto ni mama mzazi wa mtoto huyo
-----------------------
Mbunge  wa  jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe leo amejikuta  akibubujikwa na machozi baada ya  kutembelea  wodi la majeraha ya moto katika Hositali ya Misheni Rugalawa na kukutana na mtoto Diana Haule (11) mkazi  wa Shaurimoyo ambaye ameungua kwa moto mwili wake na kuimbiwa wimbo maalum uliomfanya  kutokwa na machozi.

Mbunge  huyo akiwa na familia  yake ya   mke  na watoto  wawili pamoja na viongozi  wa CCM  wilaya ya Ludewa aliofika katika wodi namba  6 ambapo mtoto  huyo amelazwa, alipokelewa kwa  wimbo maalum kutoka kwa mtoto  huyo ambao  ulikuwa  ukimsifia Mbunge  huyo. 
 
Wakati akiusikiliza na kumtazama mtoto huyo, Deo alianza kutokwa na machozi na kulazimika  kuwaomba  watu  ambao alikuwa ameongozana nao  kutoka nje ya  chumba hicho na kumuacha yeye na mtoto  huyo na watu  wachache.

Katika  wimbo  huo mtoto  huyo alikuwa akieleza  jinsi ambavyo ameshindwa  kuendelea na masomo  kutokana na tatizo na ugonjwa wa  kifafa  linalomsumbua na  pamoja na kumpongeza mbunge kwa  kufika kumjulia hali.

Kutokana na maneno yawimbo  huo, Mbunge  Filikunjombe alijikuta akiinamisha  kichwa   chini na kuanza  kutokwa na machozi huku akiendelea  kumsikiliza mtoto  huyo akiimba.

Hata  hivyo, mbali na kueleza  kusikitishwa na tatizo la Diana, bado mbunge  huyo aliahidi  kuendelea  kumsaidia Diana, pamoja na  kuisaidia  Hospitali  hiyo  zaidi.

Mtoto  huyo anadaiwa  kuungua kwa moto toka mwezi  wa tisa mwaka  huu  baada ya  kuangukia motoni wakati akiwa na mama’ke mdogo jikoni akiendelea  kuandaa chakula.

Wakati huo  huo,  Mhe. Filikunjombe amekabidhi misaada mbali mbali katika  Hospitali  hiyo yakiwemo mashuka kwa wagonjwa  wodi  zaidi ya 80, kandambili pamoja na  kutoka msaada wa chakula,  vyote  vikiwa na thamani ya  zaidi ya shilingi milioni mbili.

---
Picture

Posted by Bigie on 11:05 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.