VICENT KIGOSI AWAPA MAKAVU WABAYA WAKE.....


INAWEZEKANA ukawa unafanya kazi lakini baadhi ya watu wakawa wanaziponda kwa chuki zao, ambapo msanii anayefanya poa bongo kwenye tasnia ya filamu Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa wapo baadhi ya wasanii wenye tabia hizo na kudai kama wanaziponda kazi zake basi ni wachawi na wanachuki zao.

Mwandishi wetu alitaka kujua tabia hizo kama zipo katika tasnia hiyo, ambapo msanii huyo aliamua kuweka wazi kuwa popote penye mafanikio lazima kuwe na watu nwenye chuki huku akidai kuwa kuna wasanii wanaozichukia kazi zake kwa sababu anafanya vizuri sokoni kuliko wao.


Alisema kuwa mara nyingi watu wenye tabia hizo ni wale wasiyofanikiwa na kazi yao kubwa ni kusambaza ubaya juu ya watu wengine huku muda wao mwingine wakiutumia vibaya badala ya kubuni kazi za kufanya.


“Kuna watu wabaya sana mimi najua kuna baadhi ya wasanii ambao nipo nao karibu wanazichukia kazi zangu hasa pale zinapoenda sokoni, sijali na ndiyo maana nazidi kubuni kazi nzuri kila kukicha,” alisema.

Posted by Bigie on 9:53 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.