FILAMU YA "WAVES OF SORROW" YA MSANII RAY YAZINDULIWA KWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA VIZIWI
Posted by Bigie habari za kitaifa, ray 5:03 AMNguli wa filamu bongo Vicent Kigosi “Ray”ameendeleza utamaduni wake wa kuzindua filamu kwa staili ya kutoa msaada na safari hii amezindua filamu ya Waves of Sorrow.
Ray alikeleka zawadi katika shule ya viziwi iliyopo Buguruni Malapa, akiambatana na wasanii walioshiriki katika filamu hiyo na kufurahi na watoto hao kwa kuwagawia zawadi mbalimbali.
Ray amekuwa akifanya hivyo kila anapotoa filamu mpya kutembelea vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu au wale wenye matatizo ya kiafya.
Ray alifunguka akieleza sababu inayo mfanya kuzindua filamu zake kwa mtindo huu “Nimefurahi kuwa pamoja na watoto hawa na kuwapatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao, mara nimekuwa nikifanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa mashabiki wa kazi zangu,wakati wengine wakila na kusaza pia kuna watu hawezi kufanya hivyonami kidogo nilicho nacho nagawana na watoto, yatima ambao wana matatizo mbalimbali ikiwa ni kutoa mchango katika kuwapa moyo,”

"MIMI SI MGONJWA...NIMEKONGOROKA KWA SABABU NAFANYA MZOEZI SANA"...RAY AFUNGUKA
Posted by Bigie habari za kitaifa, ray 2:47 AM
Picha hiyo ya juu inamuonesha alivyokuwa mwanzo (kushoto) na jinsi alivyo sasa (kulia).
------------
------------
Muigizaji aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi aka Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.
Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.
Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.

WIVU WA PENZI LA MAINDA WAMFANYA RAY NA STEVEN NYERERE WAKOSANE
Posted by Bigie habari za kitaifa, MAINDA, ray 8:15 PMMASTAA wawili wenye majina makubwa ndani ya Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kuwa ni mwigizaji , Ruth Suka ‘Mainda’,
Kwa mujibu wa vyanzo makini vilivyo karibu na mastaa hao, hofu imetanda kwamba huenda wawili hao wakazama kwenye ugomvi kama ule wa Ray na marehemu Steven Kanumba.
“Ugomvi wa Ray na marehemu ulikuwa mdogo ila ulikuzwa na alipofariki dunia Kanumba kuliibuka mambo mengi sana, naomba marafiki wa dhati wa wawili hawa wakae nao ili kuweka mambo sawa,” ’ alisema mwigizaji mmoja.
Inadaiwa kuwa chanzo cha yote ni pale Steve Nyerere alipoanzisha kampuni ya kazi zake za sanaa akimshirikisha Mainda, jambo linalosemekana kumkera Ray aliyekuwa akifanya kazi na mwigizaji huyo wa kike chini ya Kampuni ya RJ Production.
“Kuna wakati eti Ray huwa hapendi kumuona mtu akiwa karibu na Mainda, mara nyingi huwa anakuwa na wivu kwa kuwa anahisi kuna kitu zaidi ya kazi,” kilisema chanzo kingine na kusisitiza kuwa Ray alimpiga ‘stop’ Mainda kushirikiana na Steve Nyerere huku suala la wivu wa kimapenzi likitajwa.
Ilidaiwa kuwa kabla ya mtafaruku huo, Steve Nyerere na Ray walikuwa ni maswahiba lakini sasa wamegeuka chui na paka na katika kutafuta ‘sosi’ ya yote hayo, ndipo Mainda akatajwa.
Vyanzo hivyo vilifunguka kuwa hali hiyo ilizua tafrani kubwa kwa kuwa tayari filamu ya Steve Nyerere (jina kapuni) ilikuwa imeanza kurekodiwa.
Baada ya kupata taarifa hizi, mwandishi aliwatafuta wahusika, wa kwanza alikuwa Steve Nyerere, alipoulizwa kuhusiana na hilo alikiri kutokea kwa ishu hiyo.
“Ni kweli mimi na Ray ni chui na paka lakini sitaweza kukwambia sababu ya ugomvi wetu kwa kuwa nitaibua mambo mengi sana, kipindi hiki nipo katika kubadilisha maisha yangu,” alisema Steve Nyerere.
Ray alipotafutwa kwa simu ya kiganjani hakupatikana na hata alipofuatwa ofisini kwake Sinza-Mori, Dar hakuwepo.
Kwa upande wake Mainda, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kuwapata wawili hao ili nao wafunguke ya moyoni mwao zinaendelea.
"SINA NDOTO YAKUOA MSANII YEYOTE....TULIZO LA MOYO WANGU NI MFANYAKAZI WA BENKI"....RAY WA BONGO MOVIE
Posted by Bigie habari za kitaifa, ray 1:45 AMKATIKA kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuwafutilia mbali wasanii wenzake, Blandina Chagula na Ruth Suka ‘Mainda’ aliowahi kudaiwa kutoka nao kimapenzi, staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi amefunguka kuwa, hatarajii kuoa msanii kwani anaogopa presha.
“Kaa ukijua kuwa sina mpango wa kumuoa staa yeyote, mwanamke ninayetarajia kumuoa ni mfanyakazi wa benki na mipango yangu ikikamilika nitakueleza kila kitu. Mimi sitaki presha bwana,” alisema Ray.
"FILAMU YA RAY IITWAYO "SISTER MARRY" YAPIGWA MARUFUKU NA MAASKOFU
Posted by Bigie habari za kitaifa, ray 4:34 AMSTAA wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta baada ya ile ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo mapadri wamemtaka asiipeleke sokoni milele.
Ishu hiyo ilitokea kwenye kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao hicho walikuwa Ray, Mkurugenzi Mtendaji wa Utamaduni aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni wa kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa.
Kikao hicho kilikuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam kumtaka msanii huyo ajieleze kimaandishi ni kwa nini mtawa Sister Marry (Irene Uwoya pichani) alikuwa akifanya matendo ambayo kiuhalisia, Wakatoliki wenyewe huwa hawayafanyi.
Kabla Ray hajajieleza kwa maandishi ndipo alipoitwa huko na kukubaliana ana kwa ana na jopo hilo huku mashinikizo kadhaa yakielekezwa kwake.
Awali, wajumbe wote wakiwa wamekaa kwenye viti, filamu hiyo yenye saa 3 iliwekwa mwanzo mwisho huku mapadri hao wakiguna kila wakati, hasa wakati Sister Marry akiwa anafanya mambo yake mabaya.
Baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, hoja zikaanza. Mwansoke akasema vipande vyote vichafu vinyofolewe na kubaki vile ambavyo wajumbe hawakuvigunia.
Baada ya bosi huyo kusema hayo, mapadri wakasema ‘noooo’. Filamu hiyo isiende mitaani hata kidogo kwani imejaa udhalilishaji wa Wakatoliki.
Inasemekana Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge Kijijini (jina halikupatikana mara moja) yeye alipigilia msumari wa mwisho kwa maneno aliyoyatoa.
Alisema kwa kuwa filamu hiyo ilirekodiwa kwenye kanisa lake hilo, anataka vipande vyote vya kanisa hilo vitolewe ndipo iingie mtaani, jambo ambalo lilimtoa machozi Ray.
Ray sasa! Siku ya Alhamisi iliyopita, Ray alizungumza na Amani na kukiri kuwepo kwa kikao hicho. Akasema itakuwa vigumu kuviondoa vipande vya kanisa hilo kwa sababu asilimia 85 ya filamu nzima imerekodiwa Maximilian Kolbe.
“Asilimia 85 ya filamu imerekodiwa Maximilian Kolbe, sasa wanaposema niviondoe ni kuimaliza filamu yote. Filamu ni ya saa 3, ukivitoa vipande vya kanisa si itabaki dakika 5 tu,” alisema Ray.
Alisema kikao kiliisha kwa maamuzi hayo, kwamba mtu wa utamaduni alisema vipande vichafu vinyofolewe huku mapadri wakitaka muvi nzima isiende sokoni na paroko wa Maximilian Kolbe akitaka kanisa lake lisionekane kwenye filamu hiyo.
Mwandishi: “Je, wewe Ray umeamuaje?”
Ray: “Sijaamua chochote kwa kweli. Niponipo tu, nimetumia fedha nyingi sana.”
"RAY HAIJUI HATA NGUO YANGU YA NDANI....NAOMBA NIWEKE WAZI KUWA SI MPENZI WANGU"...SAJENT
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, ray 9:12 AMBAADA ya ishu kuvuja kuwa msanii wa filamu Husna Idd ‘Sajenti’, ana mahusiano ya kimapenzi na ’Ray’, amezikana habari hizo huku akisisitiza kuwa msanii huyo anamchukulia kama kaka yake na suala la kutoka naye kimapenzi halina ukweli wowote.
Tukio la Sajenti kutoka na Ray lilianza kuskika pindi kundi la bongo movie lilipoenda mkoani Mwanza kucheza mchezo wa kirafiki na wasanii wa mkoani humo.
Mtandao huo ulitaka kujua Sajenti anazungumziaje habari hizo, ambapo alidai kuwa hajawahi kutoka na ’Ray’ kimapenzi na anayesambaza ishu hizo ana nia ya kumchafua ingawa alishindwa kueleza anachafuliwa kwa namna gani.
Alisema kuwa kama zingekuwa na ukweli taarifa hizo angeweka wazi lakini haoni sababu ya kukubali wakati kitu hajawahi kukifanya na wala hana wazo wa kutoka na msanii huyo kwani mpenzi wake anamtosha.
“Sijawahi kutoka kimapenzi na Ray na hajui hata nguo yangu ya ndani na kama una ukweli kama unajua natoka naye kwanini umepiga simu na kuniuliza,??.. nasema sijawahi kutoka naye,” alidai.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa kama mwanaume aliwahi kutoka naye hawezi kuficha lakini juu ya Ray atakanusha siku zote.

VICENT KIGOSI AWAPA MAKAVU WABAYA WAKE.....
Posted by Bigie habari za kitaifa, ray 9:53 AMINAWEZEKANA ukawa unafanya kazi lakini baadhi ya watu wakawa wanaziponda kwa chuki zao, ambapo msanii anayefanya poa bongo kwenye tasnia ya filamu Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa wapo baadhi ya wasanii wenye tabia hizo na kudai kama wanaziponda kazi zake basi ni wachawi na wanachuki zao.
Mwandishi wetu alitaka kujua tabia hizo kama zipo katika tasnia hiyo, ambapo msanii huyo aliamua kuweka wazi kuwa popote penye mafanikio lazima kuwe na watu nwenye chuki huku akidai kuwa kuna wasanii wanaozichukia kazi zake kwa sababu anafanya vizuri sokoni kuliko wao.
Alisema kuwa mara nyingi watu wenye tabia hizo ni wale wasiyofanikiwa na kazi yao kubwa ni kusambaza ubaya juu ya watu wengine huku muda wao mwingine wakiutumia vibaya badala ya kubuni kazi za kufanya.
“Kuna watu wabaya sana mimi najua kuna baadhi ya wasanii ambao nipo nao karibu wanazichukia kazi zangu hasa pale zinapoenda sokoni, sijali na ndiyo maana nazidi kubuni kazi nzuri kila kukicha,” alisema.

RAY AJIPANGA KUTOKA NA "WAVES OF SORROW"....
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, ray 12:12 PMLeo latest info mpya nyingine ambayo tumeipata kutoka kwa msanii huyu ni kwamba anatarajia kuachia filamu yake mpya ambayo inakwenda kwa jina la Wave of Sorrow.
Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa Bongo Movie kaa tayari kwa ujio mwingine kutoka kwa VICENT KIGOSI.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...