"UZURI WA AVRIL NDO ULIONIFANYA NIMTUMIE KATIKA VIDEO YANGU MPYA.".....DIAMOND



Ukiongelea wasichana warembo walio kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki huwezi kuacha kumtaja Avril Nyambura wa nchini Kenya. 

Ndio maana hivi karibuni brand ya Golden Rome Italian Fair iliamua kumpa deal ya kuwa cover model wa vipodozi hivyo baada ya kuvutiwa na urembo wake.


Hivyo ni wazi kwanini Diamond aliamua kusafirihadi jijini Nairobi kwenda kufanya video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Kesho’ na kumchagua Avril awe video girl. 

Bila kuficha katika mahojiano na kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Diamond alikiri kuwa uzuri wa Avril ndio uliomvutia hadi kumchagua aonekane kwenye video hiyo.

Hivi karibuni mrembo huyo alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo alikaa kwa wiki nzima na huenda walionana na Diamond na kukubaliana kufanya video pamoja.

Kwa namna nyingi video hii inasuburiwa kwa hamu kubwa ili mashabiki wa wasanii hao wote wawili waweze kuona chemistry yao. We can’t wait.

Posted by Bigie on 1:24 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.