MWANA FA ADAI KUWA SIRI YA MAFANIKIO YAKE NI MATUMIZI MAZURI YA VIPAJI ALIVYO NAVYO


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na kipaji zaidi ya kimoja ndio sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongofleva


Aliyazungumza hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama Zamani'ambapo mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo katika vituo vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho kinachompa fursa ya kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa

Alisema muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa wakati mmoja

Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika shoo

"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu niliokuwa nao " alisema Mwana Fa

Akizungumzia ujio wa wimbo wa 'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki wapate muziki ulio bora

Alisema kuwa nyimbo hiyo italeta mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki kulingana na ubora uliopo, kwani imetengenezwa 'live' kinanda, gitaa vyote vinasikika kwenye muziki huo, chini ya mtayarishaji Pfunk Majani

PRO-24 blog

Posted by Bigie on 1:38 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.