MWANA FA AITAKA SERIKALI IRUDISHE MFUMO WA ANALOGIA
Posted by Bigie habari za kitaifa, MWANA FA 7:37 AMRapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa mfumo wa digitali unawaumiza.

Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye ving’amuzi.
“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.
Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

Mwana FA akanusha kuwa na mipango ya kugombea ubunge mwaka 2015
Posted by Bigie habari za kitaifa, MWANA FA 6:57 PMRapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amekanusha tetesi kuwa ana mpango wa kugombea ubunge katika moja ya majimbo ya mkoani Tanga anakotokea na kudai kuwa lengo lake ni kuisaidia jamii lakini si kwa kupitia siasa.

Akiongea na 255 ya Clouds FM, Mwana FA amesema kwa nafasi aliyonayo kama msanii anaweza kuisaidia jamii bila ya kuwa mwakilishi wa kisiasa.
“Kusaidia jamii sio lazima uwe mwanasiasa sababu kuna watu kibao wanaofanya kama wanaharakati tu, ukasaidia ambapo kuna matatizo, kuna watu wanaweza kupandisha sauti zao wakawafanya watu wawe aware na matatizo ambayo labda walikuwa hawajayasikia na wana namna ya kuyatatua wayatatue,” alisema FA.
Akiongea na 255 ya Clouds FM, Mwana FA amesema kwa nafasi aliyonayo kama msanii anaweza kuisaidia jamii bila ya kuwa mwakilishi wa kisiasa.
MWANA FA ADAI KUWA SIRI YA MAFANIKIO YAKE NI MATUMIZI MAZURI YA VIPAJI ALIVYO NAVYO
Posted by Bigie habari za kitaifa, MWANA FA 1:38 AM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na kipaji zaidi ya kimoja ndio sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongoflevaAliyazungumza hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama Zamani'ambapo mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo katika vituo vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho kinachompa fursa ya kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa
Alisema muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa wakati mmoja
Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika shoo
"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu niliokuwa nao " alisema Mwana Fa
Akizungumzia ujio wa wimbo wa 'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki wapate muziki ulio bora

PRO-24 blog
MWANA FA AMWAGIWA "MAMILIONI" YA SIFA BAADA YA KUFUNIKA KATIKA SHOW YA FIESTA
Posted by Bigie BONGO FLEVA, FIESTA, habari za kitaifa, MWANA FA 4:27 AMKwa kujiamini kabisa, tunasema haijawahi katika historia ya Fiesta na show za muziki wa Tanzania msanii kusifiwa kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye stage kama ilivyokuwa kwa Mwana FA!
Huenda sababu ikawa ni kukua kwa mitandao ya jamii kama Twitter ambapo mashabiki wana nafasi rahisi kutoa pongezi zao kwa msanii husika lakini seriously Mwana FA aka Binamu aliangusha performance kali pengine kuliko zote alizowahi kuzifanya kiasi cha jana kwenye Twitter kugeuka mjadala na hata kuifunika show ya Rick Ross ambayo nayo ilikuwa kali sana.
Mwana FA aliingia stejini kwa plan nzuri ya namna ya kuimba nyimbo zake. Tunahisi alifanya rehearsal na maandalizi ya maana.
Akiwa na T-shirt nyekundu yenye maandishi ‘CAN’T STOP THE HUSTLE & GRIND na miwani iliyokuwa na mishikio yenye rangi nyekundu pia, alionekana smart kinoma.
FA alikuwa ameandaa nyimbo zaidi ya sita zilizohit kinoma na kuchagua kuziimba verse moja moja huku kila moja ikishangiliwa na mashabiki. Kwa kujiamini, FA aliyekuwa mcheshi muda wote aliweza kuongea na mashabiki kuliko msanii yoyote aliyepanda siku hiyo isipokuwa Rozay tu.
‘Zipo nyingi, sasa ntafanyeje?’ alisikika FA mara nyingi baada ya kuwa anakatisha nyimbo zake ili kuimba nyingine.
Unanitega, Mabinti, Binamu, Yalaiti, Habari Ndio Hiyo, Unajinua Unasikia, Naongea na wewe na zingine ziliamsha shangwe za wengi kwenye viwanja vya Leaders.
Akiongea leo kwenye kipindi cha Power Breakfast kutoa shukrani kwa wananchi kwa jinsi walivyoiunga mkono Fiesta, mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kussaga, amesema wapo wamarekani waliomfuata na kumuuliza ‘who is that guy’ wakati FA alipokuwa kwenye stage.
Kwa namna yoyote ile, performance hiyo ya aina yake ya rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma, imefungua ukurasa mwingine mpya wa heshima aliyonayo ndani na nje ya nchi na huenda ikampa michongo mingi zaidi. Kiukweli FA, amelitumia vema jukwaa la Fiesta na huo ndio tunauita ‘ukomavu’.
Hizi ni baadhi ya tweets zilizokuwa zikisifia show ya Mwana FA.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...