WALTER CHILAMBO AFUNGUKA BAADA YA NAY WA MITEGO KUMTUHUMU KUWA NI MASIKINI WA KUTUPWA
habari za kitaifa 1:55 PM
Baada ya maneno na tuhuma nzito za Ney wa Mitego dhidi ya Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012, Walter Chilambo kuwa huenda amedhulumiwa zawadi yake ya ushindi, Shilingi Milioni 50 na waratibu wa shindano hilo kwa sababu mpaka sasa yupo katika maisha duni, Msanii huyu amevunja ukimya na kusema kuwa yeye yupo vizuri kifedha.
Walter amesema kuwa maneno ya Nay hayana ukweli wowote na yeye anaishi vizuri na hadhani kama Nay wa mitego alikaa chini na kufikiria kabla ya kuongea kuhusiana na issue hii katika wimbo wake, wala hakufanya uchunguzi wowote ambao uliomhusisha yeye.
Walter amemaliza kwa kusema kuwa, Maneno haya hayamuumizi kwa vile hayana ukweli wowote, na vilevile hayawezi kumuondolea mashabiki wake.