Video: Magaidi wa ISIS Wamchinja na kumkata Kichwa Mateka Mwingine Raia wa Uingereza
news 10:42 PM
Taarifa zilizopatikana hivi punde zinaeleza kwamba kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislamu (ISIS) kimemchinja kwa kumkata kichwa, David Haines, Mwingereza mfanyakazi wa shirika la misaada, kwa mujibu wa video iliyosambazwa na kikundi hicho.
Video ya mauaji hayo ya kinyama inaanza kwa kuonyesha hotuba ya Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu Iraki, ikifuatiwa na ujumbe kwa
washirika wa Marekani dhidi ya kikundi hicho, na inahitimishwa kwa tukio
la kuogofya la kukatwa kichwa kwa Davidi ambaye ni Mskochi.
Tukio hilo limetokea na kurekodiwa katikati ya jangwa. Baada ya hotuba ya
Cameron, mtu aliyejifunga kitambaa kuficha uso huku ameshikilia kisu
anaonekana amesimama mbele ya David ambaye amepiga magoti, na kuamriwa
kusoma 'hotuba ya mwisho.'
Katika hotuba hiyo fupi, Mwingereza huyo anasema, namnukuu, "Ninapenda
kubainisha kuwa ninakulaumu Davdi Cameron kwa kuuawa kwangu.Umeingia kwa
hiari katika ushirika na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislam, kama
alivyofanya mtangulizi wako Tony Blair."
Baada ya kusoma taarifa hiyo, Davidi anakatwa kichwa kisha Mwingereza
mwingine, Alan Henning anaonyeshwa akitishiwa maisha.
Mtu aliyefanya uchinjaji huo anaonekana kuwa ni yuleyule aliyewachinja watu wengine wawili kabla ya tukio hili.
Kadhalika, anasikika akitoa onyo, namnukuu, "Iwapo wewe Cameron utaendelea kupambana na Dola ya Kiislam, basi wewe, kama bwana wako Obama, mikono yenu itakuwa na damu ya watu walio mateka wetu."
Tazama Video hapo chini( Video Inatisha)