Inaumiza Na Kukatisha Tamaa Tunapoandikwa Kwa Habari Za Uongo Kwenye Magazeti Ya Udaku: Johari


Muigizaji maarufu wa filamu Tanzania 'Johari' Blandina Chagula amsema kuwa kuandikwa vibaya na uzushi kwa mambo yanayodhalilisha ndiyo mambo yanayokwaza na kukatisha tamaa katika uigizaji.

Akizungumza na gazeti moja la kila siku lisilo la udaku Johari aliweka wazi kuwa star wa filamu nchini anahitajika kuwa na moyo mgumu kwa kuwa uzushi na mambo mbalimbali ya kusingiziwa huchangia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa kwenye tasnia hiyo waigizaji wengi wakubwa.

Johari ameyasema hayo huku baadhi ya wasanii wakiyalalamikia baadhi ya magazeti ya udaku kwa madai ya kuwaandika kwa habari za uongo na wakati mwingine hutokea pale msanii anapokuwa hakubaliani na matakwa yao katika kitu flani na kuishia kuandikwa kwa habari za kumchafua.

Posted by Bigie on 10:19 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.