Polisi yaunda timu kuchunguza tukio la bomu Songea
news 5:18 PM
Jeshi la polisi limeunda timu ya makachero kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam wakishirikiana na wa mkoa wa Ruvuma kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aliyelipukiwa na bomu maeneo ya majengo mjini songea na kujeruhi askari polisi wawili wakati akijiandaa kuwarushia askari waliokuwa doria na kisha bomu hilo kumuua mwenyewe.
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini Naibu
Kamishna wa Jeshi la Polisi Diwani Athumani aliyewasili mjini Songea
kwa helkopta kwa ajili ya tukio hilo ambalo mtu ambaye hajatambulika,
amelipukiwa na bomu na kufariki dunia wakati akijaribu kuwarushia bomu
askari waliokuwa doria na kujeruhi askari wawili PC Mselemu na WP
Mariamu Lukindo ambaye bado amelazwa hospitalini Songea.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyemtembelea majeruhi
Mariamu Lukindo ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo ni la tatu
katika mwaku huu likiwalenga askari polisi.