Patcho Mwamba Akanusha Kufumaniwa na Mke wa Mtu
news 5:26 PM
Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba amekanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni
aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye
ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe juzi
nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho
kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika
mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho