Faiza Ally awashukia wanaomkashfu Wema Sepetu na Mhe. Lowassa
udaku 10:06 PM
Mwanamitindo nchini Tanzania, Faiza Allly, ameonesha kuguswa na maneno ya kejeli wanayorushiwa Wema Sepetu na mgombea urais kwa kivuli cha UKAWA, Edward Lowassa na kuwataka watu hao kuuvaa uhusika na kuwa na hofu ya Mungu.
Amesema kuwa hakuna anayeomba ulemavu au kuomba ugonjwa fulani umpate na kudai kuwa baadhi ya watu wanaomsema mgombea urais Lowassa, kupitia ugonjwa wake ni kumkosea haki na sio uungwana.
Sambamba na hilo amesema kuwa mwanadada Wema Sepetu, hatakiwi kulaumiwa kwa kukosa mtoto lakini kubwa ni kumuombea kwani naye anatamani sana kuwa na familia yake, lakini kutokana na matatizo ambayo ni nje ya uwezo wake hadi leo hajapata familia yake.
Amesema kusambaza picha akiwa amebeba mbwa na mwanadada Zari, kuonekana amebeba mtoto ni udhalilishaji kwani kila jambo hupangwa na Mungu hakuna ajuaye kesho yake.
Amedai yeye mwenyewe aliwahi kuzushiwa kuwa na ugojwa wa Ukimwi, na kudai kuwa alijisikia vibaya sana na aliwaza endapo ni kweli angekuwa na ugonjwa huo angekuwa katika hali gani.
Amedai kuwa wanaosema vilema vya wenzao na kuficha vya kwao, wakumbuke kuwa hawawatendei haki watu hao, kwani kwa kuandamwa huko huenda matatizo yakazidi kuongezeka na kufikia hatua mbaya zaidi.
Ameongeza kuwa ni vema wakatumia kitu kingine kuweza kufikisha ujumbe wao na sio kutumia matatizo au magonjwa ya watu kwa maslahi yao binafsi.
Aidha, Mhe. Lowassa amekuwa akikashfiwa sana na baadhi ya watu wa chama tawala kwa madai ya kuwa ni mgonjwa na ugonjwa huo unampelekea kupoteza kumbukumbu na kuishiwa nguvu.
Kwa upande wa mwanadada Wema, amekuwa akishtumiwa kuwa ni mgumba na hivyo kutokana na tatizo hilo ataishia kufuga mbwa wakati wenzake wakiendelea kuongeza familia.