TID NAYE AGOMA KUSHIRIKI KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE
Posted by Bigie habari za kitaifa, TID 1:56 AMShow ya miaka 13 katika muziki ya Lady Jaydee inazidi kupata pigo baada ya TID kuwa msanii mwingine latest kujitoa kwenye show hiyo.
Moja ya sababu anayosema TID ni kuwa ana mkataba mwingine wa show unaolipa zaidi.. Sababu ya pili ni kuwa hataki kuwa katikati ya ugomvi wowote.
Hivi ndivyo alivyoandika TID kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Three reason why i can’t do lady JIDE SHOW ………….No.1 I have better contract pays me better than.
No.2 I really don’t want to be between anybody’s conflict ya kwangu yananishinda naona nieupushe shari…
No.3 nataka kuoa muda wangu ndo huu ……………kama nimekukosea captein na madame kazeni but I have been thru same shit.”
TID APEWA KICHAPO KIKALI NA MTANGAZAJI WA CLOUDS TV
Posted by Bigie habari za kitaifa, TID 8:59 AMMwanamuziki nyota wa Bongo flava ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa dansi, Khalid Mohammed ‘TID’, wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kudundwa hadi kutolewa nundu puani na mtangazaji wa Clouds TV, Cedou Ayoub a.k.a Babuu.
Tukio hilo la aina yake lililotokea wiki iliyopita kwenye kiota cha burudani Bongo pale Club Maisha na kushuhudiwa na watu kibao ambapo chanzo chake kikidaiwa ni kudaiana hela.
Chanzo chetu kilimwaga umbea kuwa, siku ya tukio hilo TID alikuwa amealikwa kwenye uzinduzi wa albamu ya mwanamuziki Country Boy iliyokuwa inafanyika mjengoni humo, ambapo baada ya onesho hilo kuisha ndipo TID akiwa ‘mitungi’ alimfuata Babuu na kuanza ‘kumzingua’.
Hata hivyo, chanzo chetu kiliendelea kueleza kuwa, baada ya walinzi wa ukumbi huo kuona hali tete ya uvunjifu wa amani waliwasihi watu hao kutoka nje kabisa ya ukumbi, huku mtangazaji huyo akiwaomba walinzi hao wawaache wapimane ubavu kidogo na walipotoka nje wakaachiwa ‘ulingo’ ndipo ngumi zilianza kupigwa.
Habari zaidi toka eneo la tukio zilisema kuwa: “Watu waliwazunguka huku wakishangilia kwa muda wa dakika tano ngumi zinapigwa ndipo maabaunsa wakawaamua, lakini, tayari TID alikuwa ameshatolewa manundu kadhaa puani.”
Aidha, kwa upande wa Babuu, alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, iliita bila kupokelewa.
Hata hivyo, watu wa karibu na Babuu walilieleza gazeti hili kuwa, kufuatia TID kuchezea mkong’oto huo, kumezuka ‘bifu’ kubwa na kuna wasiwasi wa kutekana kwa mastaa hao hivyo huku Mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba akitakiwa kuingilia kati suala hilo ili kuepusha balaa.
"WASANII WENGI WA KIBONGO WANATEGEMEA UCHAWI"...T.I.D
Posted by Bigie habari za kitaifa, TID 1:11 AMMnyama TID amefunguka kuizungumzia ‘indirectly’ scandal inayomzunguka hitmaker wa Kesho, Diamond ya kupata mafanikio kwa kutumimia waganga wa kienyeji.
Kupitia Twitter Top in Dar ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohamed alitweet kwa utani akisema, “ I really want to meet a witch doctor who can make me win big brother money ntatoa percentage we go thru a contract,Yupo?!
Tuliamua kumuuliza kama anamaanisha alichokiandika ambapo alijibu, “ am kidin mate I just heard some of them were making foolish artist look big ndo maana I make fool out it.”
Akijibu swali kama anaamini katika uchawi ama kama unaweza kumsaidia msanii asiye na kipaji afanikiwe, TID alisema, “I don’t mean nobody all I know is all this mathaf**z they don’t have talent all they have is witchcravity,huh.”
"JAPO KUNA WATU WANANIPONDA, LAKINI BIG BROTHER LAZIMA NITASHIRIKI"....T.ID
Posted by Bigie habari za kitaifa, TID 5:42 AMNia ya Khalid Mohamed aka Top in Dar kutaka kushiriki shindano la Big Brother Africa mwaka huu iko pale pale licha ya kuwepo watu walionza kumkatisha tamaa.
Kupitia Facebook TID ameandika, “A Bad Company always corrupt a good character…I wont accept that, I WILL Be in a Big Brother Superstarz.”
Mwandishi wa ripoti hii amempigia simu TID kutaka kupewa ufafanuzi wa alichokiandika ambapo amesema alimaanisha kuwa tangu Bongo5 imtaje kuwa miongoni mwa mastaa wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania katisha shindano hilo mwaka huu na watu wengi kumuunga mkono, kumetokea watu wachache wanaosema hatoweza.
TID amesema maneno hayo hayamkatishi tamaa na kwamba msimamo wake wa kuchukua fomu kujaribu bahati yake uko pale pale ambapo anatarajia kuichukua wiki hii.
“Hey bro! jst trust in urself go there n bliv t or not u gonna do smthng splendid,i adore u as wel as im ur fan so i bliv u wil do smthng so splendid and we as tanzanians we bliv in t…wsh ya ol da best, ” aliandika shabiki wake mmoja.
“As i have been buying ur albums,listening to your music,watching your videoz,come to ur show’z and many more……my positive support by VOTING alooooooooooooo……t for U@Tid Tid Topband,” aliandika mwingine.
MSHIRIKI WA BIG BROTHER WA MWAKA JANA TANZANIA ADAI KUWA "T.I.D" ANAFAA ZAIDI MWAKA HUU
Posted by Bigie BIGBROTHER AFRICA, habari za kitaifa, TID 12:56 AMMwakilishi wa Tanzania wa mwaka jana katika shindano la Big Brother Africa Julio amesema TID anaweza kuwa mwakilishi mzuri kwenye shindano hilo mwaka huu.
Julio alisema hayo jana wakati alipokuwa akitambulisha ngoma aliyoshirikishwa na Lucci, Waters Up kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM na ndipo alipoulizwa nani anafaa kushiriki katika shindano hilo mwaka huu.
“TID anafaa sana katika mashindano ya Big brother kwasababu ni mcheshi pia ni mtu mwenye sifa zote za kushiriki shindano hilo la Big Brother, ” alisema Julio.
T.I.D AMFANANISHA ALLY KIBA NA "MTU AMBAYE NI SHOGA"
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, TID 12:18 AMKhalid Mohamed aka TID mara nyingi amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kueleza hisia zake hasa kuhusiana na muziki.
Leo kupitia Facebook TID amekumbushia lile sakata la kudaiwa kupanga njama za kumuua mwanamuziki mwenzake, Ali Kiba na kumuuita ‘shoga’ yule aliyemzushia hivyo.
“Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him while am only thinkin about this Girl…No Homo,let’s make Hits,” ameandika.
Aliongeza, “Can’t forgive weak people the whole family came into my house as if I ever had any arguments before nau wat……nobody kill them.”
>>>Aliyeitwa shoga ni Ally kiba.....Rejea hii sentensi:-
"Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him "
"MZIKI WA BONGO FLEVA NI WA KIJINGA"....TID
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, TID 2:05 AMInaonekana bado mambo hayamwendei poa Top In Dar licha ya kuwa na hit ya ‘Kiuno’ hewani ambayo imeendelea kufanya poa.Hiyo ni baada ya nyota huyo ambaye jina lake halisi ni Khalid, kuamua kutumia Facebook kutoa maoni yake jinsi muziki huo unavyoenda.
“This Bongo Fleva Music is so stupid yaani kiasi kwamba we don’t even sell it only adios get sponsorship to play it lakini sisi tuko majalala,” aliandika TID.
Ujumbe huo ulivuta hisia za Chidi Benz ambaye aliamua kuchangia kwa kuandika: "Uoga. Unazaa vijana wanataka ustaa so wanakubali chochote. Wakongwe wanataka maisha so wanahitaji kuongezwa chochote. Vitu vinagongana vitu havieleweki."
Chidi aliongeza,”Watangazaji na wadau wamekua mameneja. Haikatazwi. Ila kama wewe si line yake atakupa vipi na asimpe msanii wake. We utapita vipi? Ujinga unajizaa kwa style ya mapacha."
TID naye aliongeza, “now watangazaji sasa hivi wanatutukana and they can do anything to anyone wanaweza wakasema TiD amecopy wimbo bila ya research yoyote yaani anaweza kufanya kila kitu hana limit.”
T.I.D AKITETEA "KIUNO" CHAKE
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, TID 2:54 AM
Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa muimbaji Khalid Mohamed aka Top in Dar amecopy wimbo wa Shayman uitwao Fendela Fenduze na kuupa jina la "KIUNO". Tumepata fursa ya kuzilinganisha nyimbo hizo.
Tofauti na shutuma hizo tumegundua hakuna mfanano wowote wa nyimbo hizo na kuamua kumpigia simu TID kumuuliza analizungumziaje suala hilo.
“Mimi naona tu kuna watu ambao wanataka kuniangusha. Kwasababu wameona muziki wangu unakua vizuri kwahiyo hawataki nipate advantage wananiharibia lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye amemcopy huyo jamaa wala simjui toka nilivyozaliwa,amesema TID.
“Sababu mimi sijafanya kosa lolote mimi nitakatu kimya, nitaangalia.”
Hiyo sio mara ya kwanza kwa TID kuzushiwa kucopy wimbo wa msanii mwingine kwani aliwahi pia kuingia kwenye shutuma ya kucopy wimbo wa Irmãos Verdades uitwao Amar-te assim ambao kweli ulifanana kwa asilimia kubwa.
T.I.D AIMEZEA MATE "KILIMANJARO MUSIC AWARDS"
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, TID 2:54 AMMsanii wa ‘Kiuno’ Khalid Mohamed aka Top In Dar amesema anatamani aumalize mgogoro wake na waandaaji wa tuzo za Kili baada ya mwaka 2010 kukataa kushirikishwa kwenye tuzo hizo.
“I Really want to finish my differences with Kili Music Awardz so I can pursue my dream of becoming a better Artist for my Country,” ameandika leo TID kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Sometimes in life u feel the fight is vver and seemz as tho the writings is on the wall,Superstarz u finally made bt ur picture become tainted that is wat they call Rise and Fall-Sting and Craig.”
Baada ya kutajwa kuwania tuzo za Kili mwaka 2010, TID aliandika barua ndefu kuzungumzia sababu za kujitoa kwenye tuzo hizo.
HII NDO BARUA YAKE:
“Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:
1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwenye same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!
T.I.D AJIPANGA KUTOKA NA "KIUNO" CHAKE.....
Posted by Bigie BONGO FLEVA, TID 8:15 PMMSANII mkongwe ndani ya game la mziki TID, au unaweza kumuita sauti ya pesa, ameuambia mtandao huu kuwa baada ya ngoma yake ya ‘Kiuno’ kufanya vizuri sasa anatarajia kuachia albamu ambayo itakuwa na nyimbo nane huku kukiwa na kazi nyingine ambazo hakuwahi kuziachia.
Hata hivyo alisema kuwa jina la albamu hiyo imebebwa na goma yake ya ‘Kiuno’, ambapo ngoma nyingine zitakavyokuwepo ndani ni pamoja na ‘Raha’, ‘Check Me’, na nyingine kibao kwani alishindwa kutaja majina kwa madai kuwa wasanii wa sasa wana tabia ya kuiba majina na kuyafanyia kazi.
Aliongeza kuwa albamu imeshakamilika na kitu kinachosubiriwa sasa ni uzinduzi kwani, anaamini ujio huu utamfanya aweze kurudi kwenye chati kama ilivyokuwa zamani.
Hata hivyo alisema kuwa jina la albamu hiyo imebebwa na goma yake ya ‘Kiuno’, ambapo ngoma nyingine zitakavyokuwepo ndani ni pamoja na ‘Raha’, ‘Check Me’, na nyingine kibao kwani alishindwa kutaja majina kwa madai kuwa wasanii wa sasa wana tabia ya kuiba majina na kuyafanyia kazi.
Aliongeza kuwa albamu imeshakamilika na kitu kinachosubiriwa sasa ni uzinduzi kwani, anaamini ujio huu utamfanya aweze kurudi kwenye chati kama ilivyokuwa zamani.
BAADA YA KUTOSWA KWA MIAKA MITANO MFULULIZO, HATIMAYE T.I.D APATA SHAVU LA KUPERFORM FIESTA YA DAR
Posted by Bigie FIESTA, habari za kitaifa, TID 4:17 AM
Baada ya miaka mitano bila kupata nafasi ya kupanda kwenye stage ya show za Fiesta, hatimaye Top in Dar, TID, atapanda kwenye show ya kilele cha tamasha hilo la kila mwaka, litakalofanyika October 6 kwenye viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.
Hiyo inamaanisha kuwa TID ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akijiita ‘Mnyama’ atashare stage moja na Rick Ross.
Kupitia XXL ya Clouds FM, watangazaji wa kipindi hicho wamesikika wakimtaja TID kama msanii rasmi atakayetumbuiza kwenye show hiyo.
Hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Facebook, hitmaker huyo wa ‘Kiuno’ alitoa malalamiko yake kwa kutokuhusishwa kwenye show hiyo kwa muda mrefu.
“I wiSh I coUld maKe the Guy Who does the FieSta Listing be oN my SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its Been 5 years am nt Part of It,” aliandika.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...











