"HAZIPITI SIKU MBILI BILA KULIZWA NA KERO ZA WAANDISHI WA HABARI:.....MAMA KANUMBA
Posted by Bigie habari za kitaifa, kanumba 7:17 AMMama yake mzazi na marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.
Akiongea na kipindi cha The Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.
“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.
Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku.
WASANII WAJIPANGA KUMUENZI STEVEN KANUMBA
Posted by Bigie habari za kitaifa, kanumba 3:31 AMWASANII wa filamu Tanzania wapo katika harakati za mwisho wa mchakato wao katika maandalizi ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni moja ya jambo walilokusudia kuhakikisha wanamuenzi na kuthamini mchango aliouacha kwenye tasnia ya filamu
Akizungumzia maandalizi hayo jijini Dar es Salaam rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba alisema kuwa baadhi ya maandalizi yameanza kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba, huku wakishirikiana na familia ya marehemu ili kuweka mipango ya nini kifanyike katika harakati za kutimiza lengo
Alisema kuwa lengo lao lazima litimie kwa sababu walikusudia kufanya kitu kwa ajili ya kumuenzi marehemu kutokana na mchango wake aliouacha kwenye filamu na ili kudhihirisha hilo wanaamua kumenzi katika hali ya kiupekee
"Lazima tufanye kitu cha tofauti katika kumuenzi marehemu na ili tuonyeshe upendo wetu lazima tuheshimu kile alichokiacha kwa kuendeleza" alisema Mwakifwamba
Aliongozea kuwa muda ukifika na maazimio yakipitishwa ndipo ataweka wazi ni jambo gani lililokusudiwa kufanyika
Marehemu Steven Kanumba amefariki april 7 mwaka 2012 ambapo chanzo cha kifo chake kinadaiwa kuwa ni ugomvi wa mapenzi, na aliyekuwa mpenzi wake msanii mwenzie wa filamu Lulu
PRO24
HATIMAYE MAMA LULU NA MAMA KANUMBA WAPATANISHWA
Posted by Bigie habari za kitaifa, kanumba, LULU MICHAEL 4:45 AMHatimaye mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amepatanishwa na mama mzazi wa Lulu baada ya mlolongo mrefu na mgumu wa jitihada za kuwapatanisha kina mama hao wawili.
Chanzo chetu cha kuaminika kimeripoti kwamba mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alikua mzito kupatanishwa kwa sababu ya kukasirishwa na kitendo cha mama mzazi wa Lulu ambae hakuwahi kufika msibani wala kutuma salamu za pole kwa mama Kanumba.
Baada ya Lulu kutoka kwa dhamana, mama mzazi wa marehemu Kanumba alisema yuko tayari kuonana na Lulu kwa sababu ni mtoto na hana tatizo nae lakini akasisitiza kama Lulu atakwenda kuonana nae ni sawa ila asiende na mama yake.
Wazazi hao wamepatanishwa jumapili february 10 2013 ambapo Lulu alikuepo kama muhusika mkuu wakati huo wa upatanisho, kwa siku zote mwigizaji huyu alikua akiomba kupatanishwa na mama wa Marehemu, pia alikua akisisitiza kuomba mama yake apatane na mama Kanumba,
Sababu za Mama Lulu kushindwa kwenda msibani alisema kwanza ni uoga kutokana pia na jinsi vyombo vya habari vilivyopamba, na nyingine ni machungu aliyokua nayo dhidi ya waigizaji hao wote wawili ambao alikua hajui kama walikua wapenzi, alikua anajua Marehemu anamfundisha Lulu usanii tu.
Mapatano yalisimamiwa na wazee wawili pamoja na watu wengine wa karibu wa familia na ilichukua dakika 240 kazi kumalizika kutokana na Mama mzazi wa Kanumba kuwa mgumu kiasi chake.
Baada ya kupatanishwa imeelezwa ndio mama mzazi wa Marehemu Kanumba, mama mzazi wa Lulu na watu wengine kadhaa wa karibu wa hizo familia, walikwenda kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba Kinondoni Dar es salaam.
MAMA STEVEN KANUMBA AJA NA FILAMU YA "WITHOUT DADDY."
Posted by Bigie BONGO MOVIE, habari za kitaifa, kanumba 11:52 PMMAMA Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba’ Frola Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye baada ya kuigiza katika filamu ya Without Daddy akishirikiana na watoto waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na Jamila, katika filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.
.
Ben Blanco akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
Mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika Filamu ya Without Daddy.
Mama Kanumba mwigizaji.
Filamu ya Without Daddy imeshirikisha wasanii nyota wengi kama vile Abdalah Mkumbilah ‘Muhogo mchungu’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ Cathy Rupia, Mayasa Mrisho, ‘Maya’, Othuman Njaidi ‘Patrick’ Wastara Juma ‘Stara’ Abdul Ahmed ‘Ben Blanco’ na wasanii mahiri wengineo.
.
Akiongea na FC mkurugenzi wa kampuni ya Big Daddy Production Irene Kaungwa amesema kuwa filamu ya Without Daddy ni kazi mwendelezo wa kazi ya marehemu Kanumba iliyotoka siku za nyuma ya Big Daddy na ni kazi ambayo imetentengezwa kwa ubora wa kimataifa ikiwa sambamba na kumtambulisha mama Kanumba katika tasnia ya filamu Swahiliwood.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
FILAMU MPYA YA KANUMBA IITWAYO "NDOA YANGU" ITAINGIA SOKONI TAREHE 28 YA MWEZI HUU
Posted by Bigie habari za kitaifa, Jackline Wolper, kanumba 1:56 AMWapenzi wa filamu za marehemu Steven Kanumba watakuwa na uhakika wa kumuona tena staa huyo aliyefariki April mwaka huu kwenye filamu mpya.
Filamu hiyo inaitwa Ndoa Yangu ambapo Kanumba aliigiza na Jackline Wolper.
Ndoa Yangu inatarajiwa kuingia sokoni September 28 ikiwa chini ya usambazaji wa kampuni Steps Entertainment.
Tangu kifo cha Kanumba, hiyo itakuwa ni filamu yake ya kwanza kutoka huku kampuni ya Steps ikidai kuwa imetengenezwa kwa kiwango cha juu na pia haiwezi kukopiwa kirahisi na maharamia kutokana na kutumia teknolojia ya ufungaji filamu.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...







