PICHA MBALI MBALI ZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MSIBA WA SAJUKI
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 10:39 AMPichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba akipata maelezo mafupi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba (wa pili kushoto) kuhusiana na mikakati na mipango mbalimbali ya mazishi ya Marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki,nyumbani kwao Tabata Bima,jijini Dar.Aidha kwa taarifa rasmi kutoka kwa Simon Mwakifwamba ameeleza kuwa mazishi ya marehemu yatafanyika kwenye makaburi ya Kisutu siku ya Ijumaa mapema saa tano asubuhi.Kuli kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba kuhusiana na taratibu mbalimbali kuhusiana na msiba huo,huku baadhi ya wasanii wengine mahiri wa filamu wakisikiliza kwa makini.
Mazungumzo mengine ya hapa na pale yakiendelea kufanyika kuhusiana taratibu nzima za msiba wa Sajuki,ulioko Tabata Bima,jijini Dar.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba,kushoto ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.
Baadhi ya Wasanii wa wakijadiliana jambo.
Dua ikiendelea kusomwa nyumbani kwa marehemu Sajuki.
Baadhi ya Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wakongwe wa filamu wakiendelea kuwasili nyumbani kwa marehemu Sajuki mapema leo jioni.

Watu mbalimbali wakiwe wenye simanzi kubwa wakijadiliana jambo




Watu mbalimbali wakiwa wamekusanyika kwenye msiba wa marehemu Sajuki jioni ya leo maeneo ya Tabat Bima,jijini dar.
Mdau mkubwa wa Filamu hapa nchini Saimon Simalenga akijaribu kutoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa marehemu Sajuki mapema leo jioni.
Badhi ya Wadau na Wanahabari wakiwa wamekusanyika kwenye msiba huo.
Ruge Mutahaba akisalimiana na Mkurugenzi wa ASET,Asha Baraka,pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba pamoja na Simon Mwakifwamba.
Wakifarijiana.
Vikao vikiendelea
Ruge Mutahaba akiwa ameongozana Mh January Makamba wakisalimiana na baadhi ya watu waliokuwa kwenye msiba,walipokuwa wakiwasili

Baadhi ya Wasanii wakibadilishana jambo
SAJUKI KUZIKWA IJUMAA, WAZIRI FENELLA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 9:10 AM Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwasili nyumbani kwa Marehemu SAJUKI Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.

Mke wa marehemu Wastara aliyefunikwa kanga ilikuwa ni vigumu kuamini kama mumewe kipenzi hatamuona tena alikuwa akilia muda wote na kufarijiwa na ndugu wa karibu nyumbani kwao Tabata Bima jijini Dar. kushoto ni mama wa marehemu Bi. Zaitun

Wasanii wakiwa wamejitokeza katika msiba wa mwenzao.

Watu waliojitokeza msibani huku wengine wakiwa wamekaa kwenye mitaro ya maji.
Watu wakiwa msibani huku wakijadili mambo mbali mbali. Msiba wa Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' umewagusa wengi na kuleta simanzi.

Wasanii wakiwa wamejitokeza katika msiba wa mwenzao.

Watu waliojitokeza msibani huku wengine wakiwa wamekaa kwenye mitaro ya maji.

Watu wakiwa msibani huku wakijadili mambo mbali mbali. Msiba wa Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' umewagusa wengi na kuleta simanzi.
*Marehemu Juma Kilowoko anatarajiwa kuzikwa ijumaa saa 5 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
----------------------------------------------------------
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangaraamewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt. Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ.
Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka.
Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake.
Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.
Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEN.
TASWIRA KUTOKA NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI, TABATA-BIMA JIJINI DAR
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 5:25 AMMke wa marehemu, Juma Kilowoko 'Sajuki', Wastara Juma, akiwa na simanzi nzito kwa kumpoteza mumewe.
----------------------------------------------------------------
Pichani juu ni baadhi ya taswira za waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki', Tabata- Bima jijini Dar es Salaam. Sajuki amefariki dunia leo alfajiri akiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ambapo alikuwa akitibiwa.
PRODUCER LUCCI AKERWA NA DHARAU ZA WATANGAZAJI WA BONGO
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, LUCCI 5:03 AMKupitia Twitter producer wa Tanzania aliyewahi kutengeneza beats za hits kadhaa ukiwemo Problem wa Cpwaa, Lucci amesimulia kiasi cha mtangazaji wa radio aliyejifanya kumsahau jina wakati wanafahamiana na alishamfanyia interview. Hata hivyo hajamtaja ni nani wala kitu cha radio anachofanyia kazi.
Lucci ameandika:
Aiseee jana kuna jambo limenikuta sasa sijui kama ilikua huyu radio presenter alikua HIGH KINYAMA au ni DHARAU KUPITILIZA…mtanisaidia.
Nilikua naingia supermarket jamaa akanipigia honi kama nikageuka akanipungia. I waved back. Wakati nnatoka nikamkuta nje tukaongea kidogo.
Baada ya story kadhaa na ma “long time man..upo?”..akaniomba number ili aje studio coz naye anaishi mbezi..nikampa number na kuanza kusepa.
Presenter huyu ambaye ashaa wahi kunifanyia interviews, na bata tukala wote na biti kuniomba,akatia “man..plz kama nikumbushe jina lako ivi”
Ilikua ni dharaaauuuuuu, ni kweli jina kanisahauuuuuuu, au dude was just ridiculously high on another level?!?!?
"SITAMALIZA SIKU 7 NITAKUWA NIMEAGA DUNIA"....HAYA YALIKUWA NI MANENO YA MWISHO YA SAJUKI KWA ROMA
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 4:50 AMKupitia ukurasa wake wa Facebook rapper wa 2030, Roma Mkatoliki amesimulia maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu Sajuki.
NINACHOKUMBUKA SHOW YA MWISHO ARUSHA YA KUMCHANGIA SAJUKI!!TUKIWA CHUMBANI KWAKE MIMI, WASTARA, DJ CHOKA, YUSUPH MLELA NA WENGINEO, SAJUKI ALIMSHIKA MLELA MKONO HUKU AKIMTAZAMA KWA HUDHUNI NA AKAMWABIA:
“SITAMALIZA SIKU 7 NITAKUWA NIMEIAGA DUNIA”
ILIKUWA HARD TYM SANA KWETU NA WENGI TULILENGWA NA MACHOZI KWA KAULI ILE!!
LEO LIMETIMIA LILE NENO…oooh god mfutie dhambi zake na muepushe na adhabu za huko!! nasisi tupate somo kuwa maisha yanaweza yakabadilika within a second!!Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie na apumzike kwa amani!!! poleni sana marafiki wenzangu.
Msiba wa sajuki upo nyumbani kwake maeneo ya tabata bima, na marehemu sajuki anategemewa kuzikwa siku ya ijumaa hii .yote ni kuwasubiri ndugu kutoka mkoani Ruvuma..
"NILIBADILI WANAUME KAMA NGUO LAKINI BADO SIKUFANIKIWA, MWAKA HUU SITAKI KUPENDWA"....BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 12:17 AMMSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa mwaka uliopita wa 2012 aliteswa na mapenzi kiasi kwamba hakumpata mwanaume sahihi wa kuendesha naye maisha.
Akiongelea mikakati yake mwaka huu , Baby Madaha alisema alifanikiwa katika mambo mengine lakini katika mapenzi hakufanikiwa na kumfanya abadili wapenzi na mwisho kubaki bila ya mpenzi kutokana na kushindwana kitabia na wanaume tofauti.
“Nilijitahidi sana kumpata mwanaume mwenye mapenzi ya kweli lakini sikufanikiwa, nilibaki kuumia moyo tu, hivyo mwaka huu sitaki kurudia tena ujinga huo, nimejipanga kufanya kazi zaidi na kuachana na wanaume,” alisema Baby.
SHOW YA DIAMOND YAGEUZWA UWANJA WA NGUMI NA MATUSI.....
Posted by Bigie diamond, habari za kitaifa 12:00 AMDiamond platinum amefungua mwaka vibaya baada ya show yake ya jana pale Maisha Club kumwendea ndivyo sivyo. Usiku wa Wasafi haukwenda kama ulivyokua umepangwa baada ya kutokea fujo kubwa.
Show hiyo ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza baada ya kundi kubwa la vijana wasiojulikana kuanza kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond.
Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi mpiga picha wake Bestizo Mkononi. Kuona hivyo Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.
Vitu vya thamani kama cheni,pete na camera ya Bestizo ya ThisisDiamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond kuharibika.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...





























