BABY MADAHA ALIZWA NGUO ZAKE ZA NDANI....
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 11:01 AMKATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu na muziki Baby Joseph Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa nguo zake za ndani alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni jijini Dar.
Chanzo cha habari ambacho ni shosti wa karibu wa mwanadada huyo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitiririka:
“Alizifua kama dazeni nzima hivi na kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake. Heh! Kumbe vibaka hawaachi kitu, waliruka fensi wakazichukua pamoja na ndala.”
Katika kujua ukweli wa habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Baby Madaha na alipopatikana alisema ni kweli alilizwa nguo hizo na kudai anafanya jitihada za kuhama kwani eneo analoishi limezidi kwa wizi.
JACKLINE WOLPER NA BABY MADAHA WASHIKANA MASHATI WAKIGOMBANIANA NYUMBA YA KUPANGA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa, Jackline Wolper 2:41 AMSakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
Akizungumza na mwandishi wetu, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.
“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”
KAULI YA WOLPER
Wolper alipotafutwa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.
“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli.
Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.
"UHABA WA WANAUME UMEWAFANYA MASTAA WA KIKE WATOE PENZI KWA WATOTO WADOGO"...BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 5:05 AMMSANII wa nyimbo za muziki wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Baby Madaha amewashukia baadhi ya wasanii wa kike nchini wanaojihusisha na maswala ya ngono na wanaume wenye umri mdogo maarufu kwa jina la 'Kijibwa' kuwa ni hali ya kukata tamaa na ushamba ndio unaochangia kufanya kitendo hiko
Akizungumza jijini Dar es Salaam Msanii huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wasanii hususani wa kike kujihusisha na maswala ya ngono na wavulana wenye umri mdogo huku wakitumia jina la 'kijibwa' kwa ajili ya kukidhi matakwa yao ya kingono
Alieleza kuwa hali ya kukata tamaa ndio chanzo kinachopelekea baadhi ya wasanii hao kujihusisha na maswala ya ngono na vijana wadogo huku wakijipa moyo kuwa wanatafuta faraja wakiwa na vijana hao
"Unajua hao wasichana wanaonekana kukata tamaa kwa kukosa mwanaume wanaolingana kiumri ndio maana ajimchukua mtoto mdogo na kumuhudumia kila kitu na ndipo hapo jina la 'kijibwa' linapotumika kwa kumfananisha mvulana huyo na mbwa unayemuudumia kila kitu huku kazi yake kubwa inakuwa ni kumlinda tu " aliongezea kuwa
"Kwa sababu mvulana huyo anapewa kila kitu ikiwemo kununuliwa hadi nguo yeye anakuwa na kazi moja tu hivyo hapo hamna mapenzi zaidi ya utumwa na kumsababisha mvulana huyo kukosa uhuru wa kuwa na maamuzi ya mambo yake binafsi" alisema Madaha
Kutokana na hicho kitendo Madaha alikiita ni ushamba kwa kuwa na mahusiano ambayo hayana msingi wowote ule na si kwa ajili ya mtazamo wa maisha hivyo mahusiano hayo hayaendana na mazingira ya nchi na kusababisha kudharaulika kwenye jamii inayomzunguka
Alitoa wito kwa wasichana hao wanaojihusisha na maswala hayo kuwa wanachotakiwa ni kujiamini na kujipanga upya kwa ajili ya kupambana na maisha na kutoyaogopa maisha hivyo wanachotakiwa ni kujipanga upya
PR0-24
"SHILOLE HAJITAMBUI...KUTWA NZIMA ANATEMBEA NA WATOTO WADOGO, TENA ANIKOME..!!!!"...BAY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa, shilole 12:06 AMKUTOKANA na bifu linalofukuta kama moto wa kifuu kati ya waigizaji, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’, staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameibuka na kumchana Shilole kuwa analitamani Gereza la Segerea.
Akiongea namwandishi wetu, Baby Madaha aliyelinunua sakata hilo, alimtaka Shilole kuacha kumfuatafuata shosti wake (Flora) kwani yeye hana lolote zaidi ya kuropoka maneno machafu.
“Eti Shilole anatangaza kuwa atanipiga mimi hebu ajaribu kama yeye mwanamke kweli, mimi haniwezi kamwe. Kwanza hajielewi hata thamani yake, kutwa kutembea na watoto wadogo halafu anajiona staa,” alisema Baby Madaha.
"SIJAWAHI GAWA PENZI LANGU KWA SLIM"- BABY MADAHA.
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 6:56 PMMWANADADA mwigizaji wa filamu na mwanamuziki Baby Madaha amekanusha kuwa na uhusiano na mwigizaji mwenzake wa filamu Slim baada ya habari za uhusiano wao kuvuma na kusababisha ugomvi na mzazi mwenzake Slim ambaye pia ni rafiki yake Baby Madaha, msanii huyo amedai kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na Slim bali alimshirikisha katika video ya wimbo wake tu.

Lakini jambo la ajabu rafiki yake ambaye ndio mzazi mwenzake na Slim alikasirika na kutengeneza bifu akijua anatoka naye, Baby Madaha akisema lakini pia baadae aligundua kuwa tayari rafiki yake huyo alikuwa ametengana na Slim, Madaha anasema kuwa yeye hana mwanaume yoyote na hataki mwanaume zaidi ya maisha yake ya Single
Baby Madaha
“Maneno mengi yanasemwa lakini ukweli ni kwamba sina uhusiano na Slim bali kilichotokea nilikuwa natengeneza video yangu ya muziki na nilihitaji kumpata mwanaume mwenye muonekano mzuri na mrefu kama Slim kwa hiyo kishemeji shemeji nikafanya naye kazi kama msanii mwenzangu na shemeji yangu,”anasema Baby Madaha.Lakini jambo la ajabu rafiki yake ambaye ndio mzazi mwenzake na Slim alikasirika na kutengeneza bifu akijua anatoka naye, Baby Madaha akisema lakini pia baadae aligundua kuwa tayari rafiki yake huyo alikuwa ametengana na Slim, Madaha anasema kuwa yeye hana mwanaume yoyote na hataki mwanaume zaidi ya maisha yake ya Single
"HUWA SIPENDI KUHUDHURIA MISIBA YA WATU MAANA NAOGOPA KUROGWA...!!!".BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 3:21 AMMSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa kali ya mwaka baada ya kueleza kuwa, mara nyingi hapendi kuhudhuria kwenye misiba kwa kuogopa kulogwa.
Akiongea na mwandishi wa kipande hiki , msanii huyo alisema sehemu nyingi zenye mikusanyiko ya watu ndiko wale walozi wanakofanyia kazi yao ya kuwaloga watu ndiyo maana alikacha mazishi ya John Maganga, Mlopelo, Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
“Yaani mimi siku hizi sipendi kabisa kwenda kwenye mikusanyiko ya wasanii na watu wengi kwani huko ndiko tunamalizana hivihivi kwa kulogana. Japo vifo vya wenzangu vimeniuma sana lakini sina la kufanya ila nawaombea kwa Mungu,”alisema Baby Madaha.
"NILIBADILI WANAUME KAMA NGUO LAKINI BADO SIKUFANIKIWA, MWAKA HUU SITAKI KUPENDWA"....BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 12:17 AMMSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa mwaka uliopita wa 2012 aliteswa na mapenzi kiasi kwamba hakumpata mwanaume sahihi wa kuendesha naye maisha.
Akiongelea mikakati yake mwaka huu , Baby Madaha alisema alifanikiwa katika mambo mengine lakini katika mapenzi hakufanikiwa na kumfanya abadili wapenzi na mwisho kubaki bila ya mpenzi kutokana na kushindwana kitabia na wanaume tofauti.
“Nilijitahidi sana kumpata mwanaume mwenye mapenzi ya kweli lakini sikufanikiwa, nilibaki kuumia moyo tu, hivyo mwaka huu sitaki kurudia tena ujinga huo, nimejipanga kufanya kazi zaidi na kuachana na wanaume,” alisema Baby.
MALIMBIKIZO YA DENI LA MIAKA MITATU LA KODI YA NYUMBA LAMTIA AIBU BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 6:57 PMKIPINDI hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka watu wamekuwa wakisumbuliwa na ishu kibao ikiwemo ya kodi za nyumba, ambapo hadha hiyo imemkumba msanii wa filamu na muziki Baby Madaha ambaye amepewa notes ya siku mbili awe amelipa kodi anayodaiwa ikiwa ni sh milioni mbili, za kipindi cha miaka mitatu.
Taarifa za uhakika zilizofika kwa mwandishi wetu zinasema kuwa msanii huyo hajalipa kodi zaidi ya miaka ya mitatu, huku mwenye nyumba akiwa anampa ahadi hewa kuwa atalipa kesho bila mafanikio yoyote kitu ambacho kimemlazimu mwenye nyumba kutoa makucha yake na kumpa siku hizo mbili awe amekamilusha deni hilo.
Hata hivyo taarifa hizo zinadai kuwa msanii huyo hajaonekana nyumbani hapo maeneo ya Kinondoni kwa siku tatu, lakini kutolewa kwa notes hiyo alijulishwa kwa njia ya simu.
Mtoaji wa ishu hiyo ambaye anaishi mazingira ya tukio hilo alisema kuwa baba mwenye nyumba awali kabisa alitaka kutoa vitu vya msanii huyo nje lakini kutokana na uvumilivu wake aliacha na aliamua kumpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo aondoe vitu vyake.
“Inatia aibu sana kwa msanii mkubwa kama huyo kudaiwa pesa ndogo kiasi hicho, mwenye nyumba awali kabisa alitaka kutoa vitu vyake nje lakini kutokana na hekima yake aliacha na alimpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo anamfikisha mahala husika,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta Baby Madaha ili kueleza juu ya taarifa hizo, ambapo alidai kuwa amepokea simu hiyo kutoka kwa mwenye nyumba ikimtaka kulipa kiasi hicho cha pesa, lakini juu ya kutolala ndani ni ishu ya uongo.
Alidai kuwa hajashindwa kulipa hela hizo lakini alikuwa na mipango yake anaifanya kwani hawezi kudhalilishwa kwa pesa ndogo kiasi hicho hata kama anaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Taarifa za uhakika zilizofika kwa mwandishi wetu zinasema kuwa msanii huyo hajalipa kodi zaidi ya miaka ya mitatu, huku mwenye nyumba akiwa anampa ahadi hewa kuwa atalipa kesho bila mafanikio yoyote kitu ambacho kimemlazimu mwenye nyumba kutoa makucha yake na kumpa siku hizo mbili awe amekamilusha deni hilo.
Hata hivyo taarifa hizo zinadai kuwa msanii huyo hajaonekana nyumbani hapo maeneo ya Kinondoni kwa siku tatu, lakini kutolewa kwa notes hiyo alijulishwa kwa njia ya simu.
Mtoaji wa ishu hiyo ambaye anaishi mazingira ya tukio hilo alisema kuwa baba mwenye nyumba awali kabisa alitaka kutoa vitu vya msanii huyo nje lakini kutokana na uvumilivu wake aliacha na aliamua kumpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo aondoe vitu vyake.
“Inatia aibu sana kwa msanii mkubwa kama huyo kudaiwa pesa ndogo kiasi hicho, mwenye nyumba awali kabisa alitaka kutoa vitu vyake nje lakini kutokana na hekima yake aliacha na alimpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo anamfikisha mahala husika,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta Baby Madaha ili kueleza juu ya taarifa hizo, ambapo alidai kuwa amepokea simu hiyo kutoka kwa mwenye nyumba ikimtaka kulipa kiasi hicho cha pesa, lakini juu ya kutolala ndani ni ishu ya uongo.
Alidai kuwa hajashindwa kulipa hela hizo lakini alikuwa na mipango yake anaifanya kwani hawezi kudhalilishwa kwa pesa ndogo kiasi hicho hata kama anaishi kwenye nyumba ya kupanga.
BABY MADAHA AJIUNGA NA KUNDI LA "TMK WANAUME HALISI"
Posted by Bigie baby madaha, BONGO FLEVA, habari za kitaifa, tmk wanaume halisi 4:10 AMMSANII wa muziki na filamu Baby Madaha, ameuambia mtandao huu kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitamani kufanya kazi na kundi la muziki kutoka Temeke, TMK Wanaume Halisi, hivi sasa tayari ameshajiunga na kundi hilo na anadaii atafanya muziki wake kwa moyo mmoja kwani kundi hilo halina ubabaishaji kama yale mengine aliyotaka kujiunga nayo awali.
Mwandishi wetu alimtafuta msanii huyo kuzungumzia track aliyoshirikishwa na Juma Nature inachokwenda kwa jina la ‘Narudi Kijijini’, ambapo alidai kuwa huo ni ukurasa mpya alioufungua na kundi hilo na sasa amejiunga kufanya ngoma nyingine kibao akiwa na wakali hao.
“Nimejiunga TMK Wanaume Halisi kwa sababu nawajua hawa ni wasanii ambao wanafanya kazi na si wale ambao wanakuwa na majungu majungu kwenye kazi nina imani kuwepo hapa nitafanya muziki vizuri kwani Juma Nature amekuwa akinipa ushauri sana juu ya muziki, hivyo mashabiki wangu wategemee mambo mazuri kutoka kwangu,” alisema.
Mwandishi wetu alimtafuta msanii huyo kuzungumzia track aliyoshirikishwa na Juma Nature inachokwenda kwa jina la ‘Narudi Kijijini’, ambapo alidai kuwa huo ni ukurasa mpya alioufungua na kundi hilo na sasa amejiunga kufanya ngoma nyingine kibao akiwa na wakali hao.
“Nimejiunga TMK Wanaume Halisi kwa sababu nawajua hawa ni wasanii ambao wanafanya kazi na si wale ambao wanakuwa na majungu majungu kwenye kazi nina imani kuwepo hapa nitafanya muziki vizuri kwani Juma Nature amekuwa akinipa ushauri sana juu ya muziki, hivyo mashabiki wangu wategemee mambo mazuri kutoka kwangu,” alisema.
MITUNGI YAWAPONZA NISHA NA BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa, nisha, picha za utupu 1:37 AMMASTAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na Baby Joseph ‘Baby Madaha’ juzikati walijikuta wakiingia kujisaidia choo cha kiume bila kujielewa.
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na mpekuzi wetu, ilijiri hivi karibuni katika hoteli moja jijini Dar wakati mastaa hao walipokuwa wakimpongeza Flora Mvungi kutokana na kufanyiwa sherehe ya kumtolea mahari.
Pasipo kujielewa baada ya kilevi kufika mahali pake, wauza nyago hao waliovamia gemu la muziki, walijikuta wanazama katika choo cha kiume kwenda kujisaidia haja ndogo (angalia picha hapo chini)
BABY MADAHA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI
Posted by Bigie baby madaha, BONGO MOVIE, habari za kitaifa 3:42 AM
Msanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya bongo Baby Madaha, yupo katika huzuni kubwa baada ya kumpoteza mama yake mazazi jana usiku baada ya kuumwa kwa muda mrefu.
Mwili wa marehemu unasafirishwa leo kupelekwa Musoma nyumbani kwao ambapo mipango yote na taratibu za kuzika zitajulikana huko.
Mwandishi wa mtandao huu alizungumza na Madaha ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu vingi ndani ya maisha yake.
“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,” alisema kwa maskitiko makubwa sana.
Mwandishi wa mtandao huu alizungumza na Madaha ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu vingi ndani ya maisha yake.
“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,” alisema kwa maskitiko makubwa sana.
"POMBE ILINIFANYA NIWE KIKOJOZI".....BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa 1:58 AMSTAA wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ameweka wazi kuwa suala la udokozi wa pombe alipokuwa mdogo, ndilo lilipelekea awe kikojozi.
Akifunguka mbele ya Mwandishi , Baby Madaha alisema kipindi anasoma shule ya msingi alikuwa akiiba pombe kwenye friji nyumbani na kubugia hivyo kumfanya ashindwe kujizuia usiku na kujikuta anakuwa kikojozi.
“Dah! Mama alikuwa anakasirika sana, ananichapa kishenzi bila kujua sababu kuwa ni pombe,” alisema Baby Madaha.
gpl
"SISHANGAI KUYAANIKA MATITI YANGU KWA MASHABIKI ".....BABY MADAHA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa, picha za utupu 5:39 AM
KATIKA hali ya kushangaza, msanii asiyekaukiwa matukio, Baby Joseph Madaha ameibuka na kusema ameshangazwa na kitendo cha watu kumnyooshea vidole baada ya picha zake zinazomuonesha matiti nje kuanikwa mitandaoni na gazetini.
Akizungumza na mpekuzi, msanii huyo alisema, picha hizo zilipigwa wakati alipokuwa akiwajibika jukwaani lakini pia eti haoni kitu cha ajabu kwa mashabiki wake kuziona ‘nido’ zake.

“Sasa cha ajabu nini pale? Nilikuwa jukwaani kwa bahati mbaya sidiria ikanivuka na matiti yakatoka. Ilikuwa ajali kazini ,” alisema Baby Madaha.
Msanii huyo alipokuwa kwenye tamasha moja mkoani Morogoro hivi karibuni alinaswa jukwaani akiwa amelewa huku sehemu kubwa ya kifua chake ikiwa wazi, kitendo kilicholaaniwa na wengi kwani ni kinyume na maadili ya Kitanzania.
AIBU ZA WASANII: MATITI YA BABY MADAHA YAANIKWA NJE KAMA NYANYA
Posted by Bigie baby madaha, habari za kitaifa, matiti, picha za utupu 1:36 AMSTAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amejikuta akiumbuka mbele ya mashabiki wake baada ya matiti a.k.a nido zake kuchomoza na kuonekana hadharani akiwa jukwaani na kusababisha midume yenye ukame kumzengea.
Tukio hilo la aibu isiyo na kipimo lilishuhudiwa na mwanahabari wetu usiku wa kuamkia Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako kulikuwa na tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2012.
Baby Madaha alifanya kioja hicho baada ya kutakiwa kupanda jukwaani kuimba na Juma Kassim ‘Nature’ ambaye wameshirikiana katika moja ya nyimbo zake.
Bila hiyana, Baby alipanda stejini kwa mbwembwe na kujikuta akimwaga radhi kwa kuonesha matiti hadharani na kusababisha umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe huku mwanadada huyo akiendeleza libeneke la shoo kali.
Baada ya kushuka jukwaani ndipo dada huyo alipovamiwa na wanaume wakware ambao walimbonyeza Kizenji hadi alipookolewa na mabaunsa na kupelekwa nyuma ya jukwaa.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...















