PICHA ZA RAIS KIKWETE ALIPOONGOZA MAZISHI YA SAJUKI LEO..
Posted by Bigie habari za kitaifa, KIKWETE, sajuki 6:40 AMJeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
MH. JOSEPH MBILINYI AZINDUA RASMI INTERNET CAFE YA IZZO B
Posted by Bigie habari za kitaifa, izzo b, sugu 6:09 AMRAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII- UDOM ATIWA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 15.6
Posted by Bigie habari za kitaifa 4:51 AMRAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM) IDD MOHAMED NA WAZIRI WAKE WA FEDHA IBRAHIM MATATA WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6,MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
TAARIFA TOKA KWA MDAU JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG ZINASEMA KUWA RAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII, SANAA NA LUGHA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU ANAYESOMA BCOM ACCOUNTING ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA IDD MOHAMED ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KITUO CHA POLISI UDOM KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA JANA SIKU YA ALHAMISI AKIWA NA MWENZAKE AMBAYE PIA ALIKUWA WAZIRI WA FEDHA WA KITIVO HIKO IBRAHIM MATATA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU BCOM ACCOUNTING NA KUFIKISHWA KATIKA KITUO HIKO CHA POLISI.
MARA BAADA YA KUKAMATWA WALIKUTWA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 7 LAKI 2 NA 24 ELFU.(Shilingi 7,224,000 ZA Kitanzania.) Na fedha hizo zilitolewa kwenye account ya serikali ya wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha na kupelekwa katika Akaunti ya Mtu Binafsi ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kitivo hiko Ndugu Ibrahim Matata.
Chanzo hicho kiliendelea Kujuza kuwa Awali Raisi Huyo Anahusika na kosa la kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni 1 na laki 1 katika Duka lililopo Katika Bweni namba 13 (Block 13 ).
Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa Fedha walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM tayari kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa ili kuweza Kufikishwa mahakamani
Habari zaidi ambazo Lukaza imezipata kutoka katika Vyanzo vya habari Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa fedha watafikishwa Mahakamani Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa Shilingi Milioni 15 na laki 6 ambapo waliweza kuzitoa na kuweka katika akaunti ya Waziri Wa Fedha Ibrahim Matata na kufanikiwa kuchukua Sh Milioni 7 laki 2 na Ishirini na Nne elfu ambazo ndio walikamatwa nazo Mkononi.
Hatimaye Bunge la Serikali ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii ,Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma linatarajiwa kukaa leo Saa 10 Jioni ili kuweza kutoa uamuzi wa Kumvua madaraka na kufikisha baadhi ya Ushaidi wa Sauti wakati Raisi huyo akiomba Rushwa katika Duka lililopo Block 13.
MWILI WA MAREHEMU SAJUKI UMEKWISHA ZIKWA......MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 3:56 AM
Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu

Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili.

Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar

Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi

Hapa ndipo sajuki amelala! May his soul R.I.P
"ASILIMIA KUBWA YA WANAUME WA TANZANIA WANAOKIMBILIA UBELGIJI HUISHIA KUWA MASHOGA AU KUOLEWA KABISA"...HEKA
Posted by Bigie habari za kitaifa, picha za utupu 3:39 AMKwa mujibu wa Heka Heka ya leo katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, wanaume wengi wa kitanzania wanaoenda kutafuta maisha nchini Ubelgiji huishia kuwa mashoga ama kuolewa kabisa.
Kipindi hicho kimezungumza na watanzania waishio nchini humo ambao wamesema hali ni mbaya ambapo wanaume wengi huishia kuolewa ili kuwa na maisha mazuri na sehemu ya kuishi.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, asilimia 85 ya wanaume wa Tanzania waishio nchini Ubelgiji huishia kujihusisha na vitendo hivyo hali iliyopelekea yeye ahame nchi hiyo na kwenda Marekani.
Ubelgiji ni nchi ya pili duniani kuhalalisha ndoa za jinsia moja mnamo mwaka 2003.Pia waziri mkuu wa nchi hiyo Elio di Rupo alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi za Jumuiya ya Ulaya kuapishwa kama shoga aliye wazi.
HII NDO SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU SAJUKI...
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 1:34 AM Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.
Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mwili ukipakiwa kwenye gari.

Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.



Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.




Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.

Mwili ukiondoka nyumbani.
MWILI WA MAREHEMU SAJUKI UNAELEKEA MSIKITINI KWA MAOMBEZI YA MWISHO
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 1:25 AMHII NDIO VIDEO YA P UNIT ILIYOFUNGIWA KUONYESHWA CITIZEN TV KENYA
Posted by Bigie BONGO FLEVA, habari za kitaifa, P UNIT 1:10 AMVideo ya ‘You Guy’ ambayo P Unit wametumia mamilioni kuitengeneza kupitia kwa producer maarufu wa Nigeria ambae amewahikufanya kazi na mastaa kibao wakiwemo P Square haina hata mwezi mmoja toka itoke, pamoja na kwamba imefungiwa kuonyeshwa CITIZEN TV bado inaendelea kupigwa kwenye vituo vingine.
AMINI NA LINEX WAUNGANA TENA NDANI YA "USIKU WA MTIMA WANGU"
Posted by Bigie amini, habari za kitaifa, LINEX 12:59 AMBaada ya kufanya show kali katika fainali za BSS mwishoni mwa mwaka jana na kuzua mjadala kama wapenzi hawa wa zamani wamerudiana, wasanii wa THT Amini na Linah wanatarajia kufanya show nyingine pamoja huko Kigamboni, Dar es Salaam waliyoipa jina la ‘Usiku wa Mtima Wangu’.
Show hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Club Kakala siku ya Jumamosi ya January 5 ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 6,000 tu.
Wasanii hao kwa sasa wana wimbo mpya uitwao Mtima Wangu unaofanya vizuri kwenye vituo vya radio.
TASWIRA MBALIMBALI TOKA NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI....
Posted by Bigie habari za kitaifa, sajuki 12:43 AMMazishi ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia juzi yanatarajiwa kufanyika leo mchana katika makaburi ya Kisutu baada ya sala ya Ijumaa.
Akiongea na mtandao huu, mwenyekiti wa kamati ya mazishi Steve Nyerere amesema kuwa msiba huu unasimamiwa na shirikisho na wasanii wa filamu na wadau wa tasnia hiyo.
DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU FUJO ZILIZOTOKEA WAKATI WA SHOW YAKE PAMOJA NA HASARA ILIYOPATIKANA
Posted by Bigie diamond, habari za kitaifa 10:38 PMUsiku wa january 1 2013 Maisha Club ulikua usiku maalum kwa show ya WASAFI ambao wanaongozwa na Diamond Platnums, usiku huu umeingia kwenye Headlines baada ya fujo kubwa kutokea za kurushwa chupa, viti na mayai viza.
Noma ilianza dakika 15 baada ya Diamond kuanza kuingia kwenye stage ambapo anakiri kwamba alijua kulikua kuna watu wamepanga kuja kumfanyia fujo na aliuambia uongozi wa Maisha Club mapema kwa tahadhari na wakamwambia aendelee manake wameshaongea na wahusika lakini kumbe maongezi hayakubadilisha chochote.
Anavyosema Diamond ni kwamba waliofanya fujo ni washkaji zake wa siku nyingi ambao alikua nae Kariakoo, hao washkaji walikua wamegombana hivyo kugawanyika katika makundi mawili ambapo kundi moja lilikua linataka Diamond awe nalo alafu jingine alitenge, anasema yeye alikataa hilo wazo kwa sababu wote ni washkaji zake.
Huo msimamo ulifanya hilo kundi lililomshawishi kukasirika na kuamua kulipiza kisasi kwa kufanya fujo Maisha Club, taarifa alizipata mapema kwamba wangekuja kumzomea ambapo kweli hao jamaa walipofika Maisha wakati wa show walianza kuzomea lakini Diamond akatangaza kwa mashabiki ambao walimsupport Diamond na kupiga kelele zilizowashinda hao wazomeaji ambao baada ya kuona hivyo walianza kufanya fujo.
Mmoja wa hao wazomeaji ambae aliongea na millardayo usiku huo huo kwenye eneo la tukio alisema wao hawahusiki na fujo zilizotokea, waliofanya fujo ni mashabiki tu ambao pengine walichoshwa na show ya Diamond, wao walichokuja kufanya ilikua ni kuzomea tu kwa sababu Diamond alikiuka makubaliano yao.
Makubaliano yenyewe ni kwamba kwa sababu Diamond ni mshkaji wao toka kitambo kabla hajajulikana kisanii, walishakubaliana toka wakati huo kwamba akifanikiwa kimuziki inabidi asaidie na washkaji wengine wa kundi hilo ambao ni wasanii wachanga kitu ambacho jamaa wanadai Diamond hajakifanya kabisa, siku ya tukio alitakiwa kuperform na msanii mmoja wapo aitwae Papaa Masai lakini Diamond alikataa na hicho ndicho kilichowapa hasira.
Baada ya mambo kuharibika hili kundi pia limedai kwamba kuna wakati Diamond alikua anawatuma kwenda kumzomea Bob Juniour kwenye show zake na pia alikua anawatumia kwenye show zake kwenda kumshangilia.
Diamond amesema wote waliomfanyia fujo anawajua mpaka kwa majina na tayari ameshawashitaki polisi na atahakikisha wakienda kukamatwa wanakamatwa kukiwa kuna kamera inawarekodi ili waonekane.
Kitu kingine alichokisema ni kwamba kati ya hao waliokwenda kumfanyia fujo ni pamoja na mdogo wa msanii ambae aliwahi kuwa na ugomvi nae wakapatana (huyo msanii) lakini bado huyo msanii amekua na chuki dhidi yake.
Yani Diamond aliwahi kuwa na beef na huyo msanii wakayamaliza lakini bado jamaa ana chuki, hawezi kumtaja kwa sasa na anachofanya ni kuacha uchunguzi wa polisi ufanyike kwanza, ikigundulika ni kweli atamtaja hadharani.
Kuhusu huyo msanii namkariri zaidi Diamond akisema “Uhusiano wangu na huyu msanii hauko vizuri, tulishahitilafiana kama mwaka umepita tukapatana lakini bado ana chuki dhidi yangu, tatizo niliona liliisha lakini nikaona mwenzangu kama bado ananionyesha chuki hata nikikutana nae najifanya kama hakuna tatizo lakini moyoni najua mwenzangu kuna vitu ana viendeleza vya chinichini ambavyo sivielewi”
Diamond amesema hasara ya vitu vyake kwenye hizo fujo ina thamani ya milioni zaidi ya 13 kutokana na kuibiwa simu yake ya iPhone5, cheni pamoja na camera ya video ya thamani kubwa ambayo aliinunua kwa ajili ya website yake.
CREDIT:MillardAyo
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...
















