AUNT EZEKIEL AFUNGIWA MWAKA MMOJA BILA KUIGIZA KATIKA MOVIE ZA KIBONGO


Masupastaa wawili wakubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Steven Charles Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’ wanadaiwa kuchochea kumpiga chini mcheza sinema ‘seksi’, Aunt Ezekiel Grayson kutumika katika muvi zao kwa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya sanaa hiyo, kuna kikao kilichokaa katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar kikiwahusisha waigizaji hao kilichofikia uamuzi huo huku sababu ikimumung’uywa.

Uamuzi uliofikiwa kwa mara ya kwanza ulikuwa ni kumfungia kwa mwaka mmoja, lakini ghafla waliibuka baadhi ya wasanii wakasema kama ana kosa asamehewe au afungiwe japo miezi mitatu.

Wadau walipoanza kugawanyika, muafaka haukufikiwa lakini suala la kufungiwa likabaki palepale na wasamabazaji wa filamu wa Steps Entertainment wakapelekewa taarifa,”

Walipotafutwa Kanumba na Ray kwa nyakati tofauti hawakuwa tayari kutoa ushirikiano.

Kwa upande wake Aunt alisema hajui chocho juu ya yeye kufungiwa.

Posted by Bigie on 3:08 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.